April 29, 2018

MBUNGE RITTA KABATI AMWANGUKIA RAIS DKT MAGUFULI JUU YA HOSPITALI YA FRELIMO NA MAGEREZA KUHAMISHWA , MWAMOTO AOMBA LAMI KUTOKA IPOGOLO HADI KILOLO

MBUNGE  wa  viti maalum  mkoa  wa  Iringa  Ritta Kabati (CCM )  amemuomba  Rais  Dkt  John Magufuli  kusaidia  mashine   katika  Hosptali ya  wilaya ya  Iringa Hospitali ya Frelimo  pamoja na  kuomba  gereza la Iringa  kuhamishwa mjini  kupisha upanuzi wa  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa .

Mbunge  Kabati ambae alijitambulisha kwa  Rais kama  mbunge  Kivuli wa  jimbo la  Iringa mjini  baada ya  mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa  (chadema)  kutotokea katika tukio hilo  kubwa la  ufunguzi wa barabara  ya   Iringa , Dodoma  leo  ,kuwa  yeye  kwa sasa ni mbunge  kivuli  wa jimbo la Iringa mjini   hivyo lazima   kuwasemea  wananchi  wake.

“ Mheshimiwa  Rais kama  ilivyo baraza la  mawaziri  wanaoshirikiana nawe  kutekeleza ilani ya   CCM na kuna  baraza la mawaziri  Kivuli mimi ni  mbunge  Kivuli  wa   jimbo la Iringa mjini  hivyo nakuomba  sana  nilete kwako  changamoto  za  jimbo la  Iringa mjini “

Mbunge Kabati  alisema  pamoja na  jitihada kubwa  zinazofanywa na serikali katika  kuboresha sekta ya afya na kuleta maendeleo kwa  wananchi bado  anaomba   Rais  kusaidia  Hospitali ya  Frelimo  kupata  mashine  ili  kupunguza msongamano wa  wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa .

Pia  mbunge  huyo  aliomba  Rais  kusaidia  kuhamisha  gereza la Iringa na  kulipeleka  Mlowa   nje  kidogo na mji wa Iringa  ili eneo  hilo ambalo  lipo  jirani na  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa  litumike kupanua  Hospitali  hiyo  ambayo kwa  sasa  ni  finyu  sana.

“ Mheshimiwa Rais ombi  hili  nimekuwa  nikilitoa mara kwa mara  bungeni ila  utekelezaji  wake  umekuwa  wa  kusua sua  namba  nikuombe  wewe  mwenyewe  leo  uweze  kutusaidia  ombi  letu  ili tupate  kupanua  Hospitali  zaidi “

Mbunge  Kabati  alisema  kuwa  kwa upande wa wananchi wa  jimbo la  Iringa  mjini  wanajivunia  utendaji  kazi wa Rais Dkt  Magufuli na   hasa katika  utekelezaji wa ilani ya  CCM ndio  maana kwa  sasa  jimbo  zima la Iringa mjini   hasa  wale ambao  walikuwa  upinzani  wameanza  kurejea  CCM .
 
Kwa  upande  wake  mbunge wa  jimbo la Kilolo Venance Mwamoto  pamoja na kupongeza kazi  zinazofanywa na  Rais Dkt Magufuli   bado  aliomba ujenzi wa  kiwango cha lami wa barabara ya Ipogolo -  Kilolo na pindi  itakapokamilika  basi  jina la barabara  hiyo  ipewe  jina la mtendaji mkuu wa Tanroads Mfugali .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE