April 6, 2018

MBUNGE CCM AHOJI BIBI KUVAA WIGI KWENYE NEMBO YA TAIFA
Na Ramadhan Hassan, Dodoma   |  

Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM), ameiomba Serikali ipige marufuku matumizi ya nembo ya Taifa yenye picha ya ya mwanamke na mwanamume (Bibi na Bwana) kwa sababu mwanamke huyo amevaa wigi hivyo kutoakisi maisha ya Mtanzania.
Mbunge huyo ameomba mwongozo wa Spika leo Ijumaa Aprili 6, kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ambapo amedai katika nembo hiyo kuna bwana amevaa lubega ambaye anaakisi maisha ya Mtanzania.
“Bibi aliyevaa wigi haakisi maisha halisi ya Mtanzania hivyo naiomba Serikali isitishe matumizi ya nembo hiyo na izuie isitumike hadi ifanyiwe marekebisho kwani bibi amevaa wigi ambalo haliakisi maisha ya Mtanzania,” amesema Mlinga.
Akijibu mwongozo huo Chenge alihoji iwapo tukio hilo limetokea leo hadi Mbunge huyo anauliza.
“Narudi kwenye kanuni je, suala hili limetokea leo na kama halijatokea leo halipo kwenye kanuni,” amesema.
Amesema kwa sasa wanatakiwa kuheshimu sheria inayosimamia nembo huku na kwamba njia nzuri ya kuchokoza jambo ni kuuliza bungeni.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE