April 11, 2018

MASHINDANO YA SPORT JUM YAANZA NA NEEMA ZA CCM IRINGA MJINI

Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya wa  pili  kulia  na katibu wa CCM Iringa mjini Marco Mbanga  kulia  pamoja na mwenyekiti UVCCM Iringa mjini Slvator Ngerera  wakimkabidhi pesa  kiasi cha shilingi milioni 1.5 mratibu wa mashindano ya Sport Jum Cup Saul Mbogo
Baadhi ya  mipira ya  kisasa  iliyotolewa na CCM
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya  akikabidhi  vifaa vya michezo kwa mratibu wa mashindano ya Sport Jum Saul  Mbogo  kushoto
Mratibu wa mashindano ya  Sport Jum Saul Mbogo  akipokea  vifaa vya  michezo kutoka kwa  viongozi wa CCM Iringa mjini kutoka  kulia ni katibu wa CCM wilaya  Marko  Mbanga ,mwenyekiti UVCCM wilaya ya  Iringa mjini Slvator Ngerera
Mratibu wa mashindano  hayo  akifurahia  pesa

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya  Iringa mjini Said Rubeya  akimpa  pesa mratibu wa mashindano ya  Sport Jum Saul Mbogo katikati ni  mwenyekiti UVCCM wilaya ya  Iringa mjini Slvator Ngerera akishuhudia
Mwenyekiti akimkabidhi  pesa
Viongozi wa  CCM wilaya  wakisalimiana  na  wachezaji kabla ya  mchezo kuanza  kushoto ni Shedrack na  viongozi wengine
MASHINDANO ya  kombe la Sport  Jum Iringa  mjini  yazinduliwa kwa baraka  kubwa  baada ya  chama cha mapinduzi (CCM)  Iringa mjini  kuunga  mkono mashindano hayo kwa kutoa  mipira  15 ya  kisasa na  pesa  kiasi cha shilingi  milioni 1.5

Akikabidhi  msaada  huo wa  pesa na  vifaa vya  michezo jana katika  uwanja wa  shule ya  msingi Ipogolo ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya  Iringa mjini  Said Rubeya alisema  chama kimetoa msaada  huo baada ya  mratibu wa mashindano hayo  kuomba  kusaidia vifaa na pesa kwa ajili ya  kufanikisha mashindano hayo .

Kwani  alisema  kutokana na hali  ngumu ya  uendeshaji wa mashindano hayo kwa kukosa  vifaa vya  michezo na pesa za  kununua zawadi kwa  washindi ,CCM imejitolea  kutatua  changamoto  hizo kwa kusaidia baadhi ya  maeneo ambayo  waandaaji wa mashindano hayo walishindwa  kutimiza .

" sisi  chama  cha  mapinduzi tutagharamia  zawadi ya  mshindi wa kwanza ng'ombe kama  mlivyopanga  ,pia  tutatoa  zawadi ya  mshindi wa  pili  mbuzi na mshindi wa tatu mbuzi pamoja na  kutoa  zawadi kwa mwamuzi  bora ya  mbuzi pia "

Alisema  mwenyekiti  huyo kuwa pamoja na zawadi  hizo za  ng'ombe na mbuzi wanachangia  kiasi cha  shilingi milioni 1.5  pamoja na  mipira  15  ya  kuendeshea mashindano hayo .

Mwenyekiti  huyo alisema  wajibu wa CCM ni  kuendelea  kutekeleza ilani yake na  kuwasaidia  vijana  katika  sekta ya  michezo na  kuona wanaendelea  kuienzi ilani ya CCM katika  michezo huku  akiwataka  kutumia  michezo hiyo  kuwakutanisha  vijana na kuelimishana  kuepuka matumizi ya  dawa  za kulevya .

Awali  mwenyekiti wa UVCCM Iringa mjini Salvatory Ngerera pamoja na  kuwapongeza  vijana hao  kuwa  kuwaunganisha  vijana  wote  kupitia mashindano hayo ya Sport Jum bado  aliwataka  vijana   hao  kuendeleza  michezo kwani  ni sehemu ya  ajira  hasa  ukizingatia  kuwa mkoa wa Iringa kwa  sasa  umeendelea  kufanya  vema katika michezo kwa  kuwa na  timu  zinazocheza  ligi kuu Tanzania  bara .

Ngerera  alisema  kuwa siku  zote  ndani ya  CCM  kuna  dawati maalum kwa  ajili ya  kuwasikiliza  vijana na kero zao   hivyo  wasisite  kufika  kuwashirikisha  changamoto  zao na  zile  ambazo  zipo ndani ya  uwezo wa chama  zitatatuliwa .

Mratibu wa mashindano hayo  Saul Mbogo  alisema  kuwa  mashindano hayo  yanashirikisha  timu zaidi ya 30 kutoka  wilaya  nzima ya  Iringa mjini  na  kupngeza  CCM Iringa mjini  kwa  kusaidia mashindano hayo .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE