April 24, 2018

MANISPAA YAWA MFANO YATUMIA ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI KUTOA MIKOPO YA MILIONI 140 KWA VIKUNDI

Mstahiki  meya  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  Alex  Kimbe kushoto  akikabidhi mfano  wa  hundi kwa  wanakikundi Makorongoni baada ya  Halmashauri  hiyo  kutumia  asilimia  10 ya  mapato ya  ndani  kutoka  mikopo kwa  vijana na  wanawake  Diwani wa kata ya Mlandege  Amani Mwamwindi  akitoa  salam  zake 
Madiwani  wa  viti maalum  Chadema  Iringa  wakiwa na madiwani wa CCM 
Baadhi ya walengwa wa mikopo ya Manispaa ya  Iringa  
vikundi  mbali mbali  vilivyonufaika na  mikopo  ya Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa .
Diwani  wa Mshindo  Ibrahim Ngwada  akitoa  neno 
Mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  akizunguza katika   hafla  hiyo 
Meya  Kimbe  akiteta  jambo na Dc  Kasesela  kulia 
Mwakilishi wa Ewura  akitoa  semina kwa  wanavikundi 
Taarifa  ya  mikopo  ikikabidhiwa 
Wanakindi  wa  Mivinjeni  wakipewa  mkopo  huo

...................................................................................................................................
HALMASHAURI  ya  Manispaa ya  Iringa  mkoani  Iringa  imekuwa ni moja kati ya  halmashauri  za mfano  katika mkoa  wa  Iringa kwa  kutumia asilimia  10 ya  makusanyo  ya  ndani  kutoka mikopo  yenye  thamani  ya  shilingi  milioni 140  kwa  vikundi  vya vijana na  wanawake.

Akikabidhi   mikopo  hiyo  leo katika  hafla  fupi  iliyofanyika  ukumbi wa  Olofea  mjini hapa  mstahiki  meya  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Alex  Kimbe  alisema  mkopo  huo   hauna  mahusiano na  pesa  za  ahadi ya  Rais  Dkt  John Magufuli ya  shilingi  milioni 50  kila kijiji bali  hizo ni  fedha  zilizotokana na makusanyo ya  ndani ya Halmashauri  hiyo  ambayo  yanaitaka  halmashauri  kutumia  asilimia  10  kutoa mikopo kwa  vijana na wanawake .

 Meya  Kimbe   alisema  kuwa  Halmashauri  ya  Manispaa ya  Iringa  imeendelea  kutoa  mikopo  kupitia  makusanyo yake ya ndani  na  kuwa  njia pekee  kwa  wananchi na  wafanyabiashara  kuendelea  kulipa  kodi.

Alisema  kuwa  katika  kipindi cha  mwaka  2017  hadi 2018 halmashauri  ya  Manispaa ya  Iringa  imetenga kiasi  cha  shilingi  418,082,700 ambayo  ni  asilimia  ya  mapato  yake ya ndani  kwa  ajili ya  kutoa  mikopo  kwa  vikundi  vya  vijana na  wanawake  kiasi cha shilingi 209,041,350 imetengwa  kwa  vikundi  vya  wanawake  na  shilingi 209,041,350 imetengwa  kwa  vikundi  vya vijana .


Katika awamu ya  kwanza ya  mwaka  2017/18 Halmashauri  ilitoa  kiasi cha  shilingi  110,000,000 ikiwa  ni sawa na asilimia 26 ya fedha iliyotengwa kwa  ajili ya  kukopesha vikundi  vya  vijana na  wanawake   na kuwa idadi  ya  vikundi  36  vya  vijana  na wanawake  vilinufaika  ikiwa ni vijana  vikundi  12  na wanawake  vikundi 24.

Hata  hivyo  alisema katika  kipindi cha robo ya tatu  ya mwaka 2017/2018 pekee Halmashauri  imetoa  kiasi cha  shilingi milioni 140 kwa vikundi 42 vya wanawake  na  vijana  .

Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 100,500,000 kimetolewa kwa vikundi  30  vya wanawake  ambayo ni sawa na asilimia 48 ya fedha  iliyotengwa  kwa  ajili ya kukopesha  vikundi  vya wanawake  na  kiasi cha  shilingi milioni 39,500,000 kimetolewa  kwa  vikundi  12 vya  vijana ambavyo ni sawa na asilimia 19  ya  fedha iliyotengwa  kwa  ajili ya kukopesha vijana .

Kimbe  alisema  wanachama  437 watanufaika  kati yao  wanawake  361 na  vijana ni 76 ambao  watafikiwa na  mikopo  hiyo  iliyolengwa  kuwakwamua  vijana na  wanawake .


Afisa  maendeleo  ya jamii  Manispaa ya  Iringa  Aliah Kasanga  alisema pamoja na  kuwepo  kwa mafanikio  makubwa katika utoaji wa mikopo  hiyo na  wanawake  kuwa  mfano katika  urejeshaji  shida  ya  urejeshaji  wa  mikopo  ipo kwa vijana .

Awali  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  pamoja na kuipongeza Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa kwa  kutoa  mikopo  hiyo kwa  vijana  na wanawake bado  aliwataka  walengwa  kutumia  mikopo  hiyo kwa lengo la  kujikwamua  kiuchumi  badala ya  kutumia mikopo  hiyo  kufanya  starehe .
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE