April 20, 2018

MAKOCHA LIPULI FC : SIMBA KUTUPANDISHIA CV ZETU HACHOMOKI , CLEMENT SANGA AMPA NENO MANARA KUWA AJIANDAE KULIA


 Makocha  wa Lipuli FC  Seleman Matola (kushoto)  akiwa na kocha msaidizi Amir Said wakionyesha ishara  ya umoja  na ushindi kesho  timu  ya  Lipuli Fc itakapocheza na Simba Sc uwanja wa  Samora.
WAKATI  kesho   timu ya  Lipuli  FC  ya  mkoani Iringa maarufu kama wanapaluhengo  inawakaribisha  Simba SC  katika uwanja  wa Samora  mjini  Iringa  ,kocha  mkuu wa  Lipuli Fc  Selemani Matola na kocha  msaizidi wa  timu  hiyo Amiri  Said  wamesema leo  wanatafuta  kupandisha CV zao kwa  'kukuigagadua ' Simba Sc kwenye  uwanja  huo wa   ambao ni uwanja  wa Nyumbani kwa Lipuli FC .
Huku  msemaji wa  Lipuli Fc Celent  Sanga  akimpigilia  nyundo  msemaji wa  Simba  Sc Haji Manara   kuwa kote  timu yake ilikocheza  ametoka  akifurahi na  kucheka  kwa  Lipuli  Fc ajipange kununa na kutoka akilia baada ya  dakika 90  za  mchezo.

Wakizungumza mtandao wa matukiodaimaBlog na matukiodaimaTV leo  kuhusiana na maandalizi ya mchezo  huu wa  kesho  makocha hao   walisema kuwa   pamoja na  kwamba mchezo  huo ni mgumu kwa timu  zote  mbili  ila wao kama wenyeji  wa uwanja wa Samora hawatakubali  kuona  wanashusha  CV zao kwa  kufungwa na  Simba Sc .
Image result for Lipuli Na  simba
Matola  alisema  kuwa timu  yake  imejipanga  vema  kuona  inautumia  vizuri  uwanja wa  Samora kwa  kutafuta  pointi tatu  za  mchezo  huo  kutoka kwa  wageni  wao  Simba Sc .

" Kuna  maneno ambayo  yanasambazwa  katika  mitandao ya  kijamii na mitaani  kuwa Lipuli Fc ni tawi la  simba  tunaomba  sana mashabiki  wa  Lipuli Fc kuyapuuza kwani kama Lipuli Fc  ingekuwa ni tawi la  simba  tusingetoka  sare   tulipo kutana katika uwanja    wao   nyumbani uwanja  wa  Taifa "

Alisema kuwa maneno hayo yanaongelewa  tu kwa watu  kujifurahisha  kwani  toka  ligi  imeanza  timu ya  Simba  Sc  haijapata  kupoteza mchezo hata  mmoja  zaidi ya  kutoka  Sare  ila  wao  wanataka  kuwa    walimu  wa kwanza  kuweza  kuifunga   Simba ili  kuweza  kutengeneza  CV zao kama  walimu nguli  ambao hawajafungwa  na  simba toka  ligi ianze .

Kwa  upande  wake kocha msaidizi wa  Lipuli Fc Said  alisema  kuwa  hajapata  kuona   kuona kama  Lipuli Fc ni tawi la  simba Sc  ila anachotambua  Lipuli Fc ni  timu kama  zilizo timu  nyingine  zote  zilizopata kukutana na   Simba hivyo  wanaodhani  Lipuli Fc ni tawi la  simba  wafike Samora  kesho jumamosi ili  kuona kama ni tawi  ama ni  timu inayojitegemea .


"Kumfunga  Simba  ni CV na  kutoka  sare na  Simba ni  CV pia  maana ni  timu ambayo kwa  miezi hii miwili  ndio  imeonyeshakuwa ni timu  yenye  uwezo  kwa  kucheza  vizuri na  kuwa na washambuliaji wazuri  na ni miongoni mwa  timu zenye  kocha  mzungu  ila  mimi na kocha mwenzangu  tumejipanga  kupaisha  CV  zetu  iwe kwa  kuifunga ama kutoka  sare lazima  historia  iandikwe  kesho uwanja wa  Samora "

Alisema  kuwa  Lipuli  FC  inaingia  uwanjani kama timu  iliyojipanga  kufanya  vizuri  kama ilivyofanya  jijini Dar es Salaam  ndicho  kitakachofanyika  sasa  tunahakikisha  tunapata  pointi tatu ama  mbili au  pointi  moja ya  sare .


" Mashabiki  wa  Lipuli Fc watuamini  walimu pia  waiamini  timu  yao timu  yetu ya  Lipuli Fc ni  nzuri  na imejipanga  kufanya  vizuri katika  mchezo  huu na  Simba vijana  wetu  wapo  vizuri kiafya na kimchezo  ushindi ni  lazima "

Msemaji  wa    timu ya  Lipuli  FC Clement  Sanga alisema  kuwa  jambo la  msingi ni kwa  wana Iringa  kujitokeza kwa wingi katika  uwanja  wa  Samora kuishangilia  timu yao ya  Lipuli na  kuwa isingependeza  kwa  wana Iringa kuonyesha  Usimba ama  Uyanga  katika mchezo huo  ambao kwa  pamoja  wana Iringa wanaamini nyumbani ni  nyumbani na Lipuli Fc ni kiunganishi cha  wote .

" Wana Iringa  wote  wanapaswa  kutembea  kifua mbele  kwa kuvaa sare  kila mmoja  sare za simba  tunaonyesha  uzalendo  mkubwa na  kuwa  Lipuli  Fc ndio  timu pekee  mbabe wa  simba Sc "

Sanga  alisema  kuwa hakuna  wakati  mzuri kama  wa  sasa ambao  timu  ya  Lipuli Fc  inacheza na  Simba   huko kila mkazi wa Iringa akiwa na shauku  kubwa la  kushuhudia Simba Sc ikilalaliwa vikali .Image result for Msemaji wa  Simba  akilia

 "Tunaikaribisha  Simba  katika  uwanja  wetu wa kujidai  uwanja  wa  Samora  na  ninamkaribisha  sana Haji  Manara  maana  kote  alikopita  alikuwa ni mtu wa  furaha  na  kicheko kwa  Iringa ataondoka na majonzi  kwani Lipuli Fc ndio  wababe wa Simba Sc "
Image result for Msemaji wa  Lipuli Fc

Wakati  huo huo mashabiki wa Lipuli  Fc  wameeleza  kusikitishwa na bei kubwa ya jezi ambayo  imekuwa ikiuzwa  kwa  jezi shilingi 20,000  kuwa ni  kubwa  ukilinganisha na  bei  za  jezi  za  timu  nyingine na  kuwa ilipaswa  jezi  kuuza kama  jezi  za timu  za Yanga na Simba   ili  kuwawezesha  mashabiki  wengi  kuvaa jezi  za  timu yao  uwanjani  na  ingewezekana  kutengeneza  jezi za kiwango cha  chini na kuuza  shilingi 10,000 alisema Peter John .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE