April 28, 2018

HALMASHAURI MJI MAFINGA YAKOPESHA VIJANA NA WANAWAKE ZAIDI YA MILIONI 126.7


Image result for Mkurugenzi mji Mafinga  SaadaHALAMSHAURI ya  mji Mafinga  mkoani Iringa imetumia asilia 10 ya makusanyo yake na ndani pamoja na marejesho ya mikopo  hiyo kukopesha vijana na  wanawake  zaidi ya  shilingi milioni 126.7

Akizungumza na  waandishi  wa habari jana  mkurugenzi wa Halmashauri ya  mji Mafinga  Saada  Mwaruka  alisema  kuwa mikopo  hiyo  imetolewa   ikiwa ni  sehemu ya  utekelezaji wa agizo la  serikali ya Dkt  John Magufuli   katika  kuwawezesha  vijana na  wanawake .

" Halmashauri ya  mji Mafinga  ili kutimiza  azimio la  bunge  la mwaka 1993/1994  na  serikali ya Dkt Mafuguli imekuwa ikitekeleza  agizo la serikali   la kutenga  asilimia 10 ya mapato  yake  ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo  yenye mashariti nafuu  kwa ajili ya  kukopesha  vikundi  vya  wanawake na  vijana  ili kuwawezesha  kuongeza  mitaji yao"

Alisema katika  kipindi cha mwaka 2017/18 Halmashauri ya mji  wa Mafinga  ilitenga  kiasi cha  sh  275,143,570  ambayo ni asilimia  10  ya mapato ya  ndani  kwa  ajili ya kutoa mikopo kwa  vikundi  vya vijana na wanawake .

 Katika  awamu ya kwanza  2017/18 halmashauri  ilitoa kiasi cha sh 76,000000 iliyotengwa  kwa  ajili ya  kukopesha  vikundi vya  wanawake na  vijana  idadi ya  vikundi   vya  wanawake 40  na vijana 20  vilipata  mkopo  huo .


 Mkurugenzi   huyo  alisema kwa  kipindi cha  robo ya tatu ya tatu  Halmashauri ya  mji Mafinga  imetoa  mikopo  yenye  thamani ya   sh. 50,700,000  katika  fedha  hizo   Tsh 14,000000 ni fedha  zilizotokana na mapato  ya  ndani na  milioni 36,700,000 ni fedha  zilizotokana na marejesho ya mikopo  iliyokopeshwa ambapo  vikundi vilivyokopeshwa  vijana  ni  vikundi  18 walikopeshwa   sh 22,000,000 na  wanawake vikundi 27  walikopeshwa Tsh 28,700,000
 
Hata hivyo  alisema halmashauri ya  mji  Mafinga    ina  vikundi  vya  wanawake 124  vyenye  jumla  ya  wanachmama 1091  na  vijana 56  wakiwemo  wanaume 384 na   wa  kike 270 jumla  yote na 
654 na  wanufaika   wote  1745.
 
Akizungumzia   mafanikio ya   vikundi  hivyo alisema vikundi vimeweza  kukuza  mitaji yao na kuwa na uchumi  mzuri kutokana na  mikopo  hiyo pia baadhi ya wanawake   wameweza  kubadilisha  maisha yao kwa  kusomesha  watoto   na idadi  kubwa ya  wanawake na  vijana  wamezidi  kuongezeka  kujiunga na  vikundi

Kuhusu  Changamoto  za  vikundi hivyo alisema urejeshaji  wa  mikopo  umekuwa  ukicheleweshwa  hivyo  kukwamisha  wahitaji  wengine  kunufaika na  mikopo  hiyona baadhi ya  vikundi  kutoonyesha  uaminifu wa kutumia  fedha   hizo za  mikopo  kufanya  shughuli  nje ya zile walizoombea   mikopo  hiyo
 
  Hata  hivyo alisema  halmashauri  imeendelea  kutembelea  vikundi  hivyo pamoja na  kutoa  elimu ya matumizi  sahihi ya  mikopo wanayopewa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE