April 23, 2018

HALMASHAURI IRINGA ZABANWA NA TAKUKURU MIRADI NANE YA MAJI NA BARABARA ILIYOTUMIA BILIONI ZAIDI YA 2.5 KUCHUNGUZWA


Kasmanda  wa  taasisi ya  kuzuaia  na kupambana na  rushwa  (TAKUKURU)  mkoa  wa  Iringa  Aidan  Ndomba  akizungumza na  wanahabari  leo  ofisini  kwake 
Baadhi ya  maofisi  wa  Takukuru  mkoa wa Iringa  wakifuatilia  taarifa   hiyo .


Na MatukiodaimaBlog

TAASISI   ya  kuzuia na  kupambana na  rushwa  nchini (TAKUKURU)  mkoa  wa  Iringa  imechunguza  miradi  nane ya  sekta ya elimu ,maji na barabara  yenye  thamani  ya  takribani  bilioni 2.5 katika  wilaya ya Iringa , Mufindi na  Kilolo baada ya  kuwepo kwa dalili  ya matumizi mabaya ya  fedha  za  za  miradi hiyo .

Kamanda  wa Takukuru  mkoa wa Iringa Aidan  Ndomba  amewaeleza  wanahabari  ofisini kwake  leo wakati  akitoa  taarifa ya utendaji kazi wa  Takukuru  mkoa wa Iringa kwa  kipindi cha JUlai  hadi Desemba  2017  alisema  ndani ya  kipindi  hicho  ofisi yake  ilifuatilia  na  kufanya  ukagzi  wa fedha  za  miradi  nane  ya maendeleo  katika  sekta za elimu ,maji na barabara  yenye  thamani ya  takribani shilingi bilioni  2,588,000,000 na kubaini mapungufu  katika  miradi yenye thamani ya  shilingi milioni 818 ambapo  uchunguzi  wa matumizi ya  fedha  za  miradoi umeanzishwa .


Alisema  kuwa  miradi  miwili  ilifuatiliwa  na kukaguliwa  katika  Halmashauri ya  Iringa na  ina  thamani ya   shilingi  1,164,614,899 iliyopo  katika kijiji  cha Mfyome   kata ya  Kiwere   na  Malizanga  kata ya  Mlowa   huku miradi mitatu  iliyofuatiliwa   na  kukaguliwa ipo  katika  Halmashauri ya  Kilolo ina  thamani ya shilingi 908,138,034 kuwa  miradi hii ipo  kijiji  cha Ng'uruhe , Irindi, na Ipalamwa .


 Kamanda  huyo wa Takukuru  mkoa wa Iringa alisema kwa upande wa barabara  miradi miwili ilifuatiliwa  na kukaguliwa  katika  wilaya ya  Mufindi  na ina thamani ya  shilingi 407,343,774 na kuwa miradi hiyo ni pamoja na barabara  za Maduma  -Tambalang'ombe  na Maguhani - Udumka .

wakati kwa  wilaya ya  Kilolo kuna  mradi  mmoja  wa barabara   wenye  thamani ya  shilingi  107,343,774 umefuatiliwa na  kukaguliwa  mradi huu ni ule wa Ilula  ujulikanao kama  KItelewasi - Ilambo .

Taasisi   hiyo imesema  kuwa   kwa  kipindi cha Julai  hadi  Desemba 2017   ilipokea  jumla ya  malalamiko  91 ya  rushwa  na kati ya hayo  malalamiko 29 yalifunguliwa  majalada  ya  uchunguzi  na malalamiko 62 yalifunguliwa  uhunguzi  wa awali  na kutolewa  ushauri  kwa  walalamikaji  ama  kuhamishiwa idara  nyingine.


Alisema  kuwa  baadhi ya  sekta  zilizolalamikiwa  ni  pamoja na  TAMISEMI ( Halmashauri  na  serikali  za  mitaa,vijiji  )   kwa  kuwa na malalamiko 18  , jeshi la  polisi  malalamiko  12 na  mabaraza  ya  ardhi malalamiko 8.

Kamanda  Ndomba  alisema  jumla ya  mashauri  mapya  matatu  yalifunguliwa  mahakamani  kwa kipindi hicho  na  kufanya jumla ya mashauri 9  kuendeshwa  katika  mahakama .

Aidha  alisema  mashauri  mawili  yalikamilika  kwa  kutolewa  hukumu  katika shauri  namba  CC 03/2017 kati ya  Jamhuri na  Upendo Mponzi  (VEO- Ilula)  na  mwenzake Tulinutwa  Alphonce  Mlangwa  ambae  ni  diwani wa  kata ya  Kipaduka wote  wakiwa ni  watumishi  wa   umma  hakimu wa  mkoa  wa Iringa John Mpitanjia  aliwatia  hatiani wote  na  kuhukumiwa  jela miezi 6 ama  kulipa faini ya  shilingi 300,000 kila  mmoja .

Pia  alisema katika  shauri  la  pili  namba CC.39/2016 mshtakiwa  Selemani Futani  ambae ni mfamasia  msaidizi  wa Halmashauri ya  Mufindi aliachiwa   huru  na mahakama  ya  wilaya ya  Mufindi  hata  hivyo upande  wa Jamhuri  (Takukuru)  wamekata  rufaa mahakama kuu .

Kamanda  Ndomba  alisema kwa  kipindi  hicho  Takukuru  mkoa  wa Iringa imefanikiwa  kuokoa  kiasi cha shilingi 100,000 baada ya  kubaini  kuwa  kiasi hicho  cha fedha  zilikuwa  zilipwe mahakamani  kama  faini zilitumiwa na mtumishi  binafsi  wa mahakama  badala ya  kuziingiza  kwenye  mfuko  wa serikali .
Hivyo  amewataka  wananchi  kuendelea  kufika  ofisini kwake ama  ofisi  za wilaya   kutoa  taarifa  mbali mbali za  rushwa ama  kutumia  simu  0784606519/0754606519 ama  kupiga  simu ya  bure 113 au  *113# kupitia  huduma ya longa  nasi kwa ujumbe  mfupi SMS 113

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE