April 25, 2018

DIWANI WA KATA YA NDULI AFANYA MAKUBWA KATANI AJITOLEA GARI LA SHULE

Usafiri wa wanafunzi shule ya sekondari Nduli jumbo la Iringa Mjini uliotolewa na Diwani Bashir Mtove (CCM) kwa matumizi ya wanafunzi
Mtavangu akikabidhi funguo ya gari hilo
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Nduli
Diwani Bashir Mtove wa tatu kulia akipongezwa kwa msaada wake wa gari la shule.
Baadhi ya wadau wa maendeleo Nduli wakiwa na familia iliyokarabatiwa nyumba na Diwani Mtove ,wa kwanza kushoto aliyekuwa Diwani wa kata ya Kwakilosa Joseph Lyata aliyehama chadema na kujiunga CCm ,Mtove,na madiwani wa Miyomboni Kitanzini na familia iliyosaidiwa.
,.................................................
Na MatukiodaimaBlog
DIWANI wa kata ya Nduli katika jimbo la Iringa mjini Bashir Mtove ( CCM)ametumia zaidi ya shilingi milioni 7.5 kutatua chamoto kwenye kata yake ikiwa ni pamoja na ununuzi wa  basi la shule  kwa ajili ya wanafunzi sekondari ya kata ya Nduli.

Mtove amechukua uamuzi wa kununua     basi hilo la shule  kutokana na adha kubwa ya usafiri  ambayo wanafunzi wa sekondari ya  Nduli walikuwa wakiipata kwa kutembea zaidi ya kilomita 32 kwa kwenda na kurudi kila siku.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi basi hilo la shule lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 22 Leo alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo ili kuepusha adha ya usafiri kwa wanafunzi wa shule hiyo hasa wale wanaotoka vijiji vya mbali na shule hiyo.

 Kwani alisema shule ya sekondari Nduli ni shule ya kata na baadhi ya wanafunzi wanatoka mbali na shule hiyo na hulazimika  kuamka saa 9 alfajiri kila siku kuwahi shule.

"Kati ya wanafunzi 580 waliopo shuleni hapa baadhi yao wanatoka vijiji vya Msisina,Mtalagala na njiapanda zaidi ya kilometa 32 kutoka shuleni hapo hutembea kila siku kwenda na kurudi "

Hivyo alisema pamoja na usafiri huo utawasaidia kufika shule kwa wakati ila bado utawaondolea mazingira hatarishi wasichana kushawishiwa na madereva bodaboda na hata kukomesha matukio ya ubakaji kutokana na mazingira wanayotoka.

Diwani Mtove alisema kuwa kwa ajili ya kutatua changamoto za watoto wa kike kutembea mwendo mrefu wapo katika mchakato wa kutafuta wahisani ili kujenga bweni la watoto wa kike japo watoto 80 kwa kuanzia.

Hivyo alisema jumla ya zaidi ya shilingi milioni 140 zinahitajika kujenga bweni hilo.


 Wakati huo huo Mtove amekabidhi nyumba kwa mmoja kati ya wajane kata ya Nduli iliyokarabatiwa na kufunikwa bati mpya baada ya nyumba hiyo kuezuliwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

 Alisema nyumba hiyo imekarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni 1.5 na basi hilo dogo la shule aina ya Hiace limenunuliwa kwa shilingi milioni 6 na kufanya jumla yote kufikia milioni 7.5


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE