April 27, 2018

DC KILOLO AWATUPA MAHABUSU VIONGOZI WA KIJIJI CHA IFUWA KWA UFISADI WA ARDHI ,AAGIZA DALALI MSUNGU AKAMATWE POPOTE ALIPO


 Mwenyekiti wa  kijiji cha Ifuwa  kata ya  Udekwa Lasta Chavaligunga  akiwa  chini ya  ulinzi  wa  polisi
 Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  akiwa na ulinzi wa  kutosha  wakati  akifuatilia  ufisadi wa ardhi  kijiji  cha Ifuwa  kata ya  Udekwa
 Mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah akiwasili  kijiji  cha Ifuwa  kupambana na  ufisadi wa ardhi na kamati yake ya  ulinzi na usalama
 katibu wa itikadi na uenezi  CCM  wilaya ya  Kilolo  Remy  Sanga  akitoa neno

 wananchi  wa  kijiji  cha Ifuwa  wakishangilia uamuzi wa  mkuu wa  wilaya  ya  Kilolo  kuagiza  mwenyekiti wao wa  kijiji  kukamatwa na  polisi
 Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akitoa  agizo la  mwenyekiti wa kijiji  na  wenzake  kukamatwa ,kushoto ni  mwenyekiti aliyekamatwa na  polisi kwa  tuhuma  za  uuzaji wa ardhi  kienyeji 
 Mwanamke  mkazi wa  Kilolo  kijiji cha Ifuwa  akimweleza  jambo la  siri  mkuu wa wilaya ya  Kilolo

 Wazee  waliotapeliwa  maeneo yao  na  mwenyekiti wa  kijiji  wakizungumza na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo
 Mwenyekiti wa  kijiji  cha  Ifuwa  akiwa  chini ya  ulinzi wa  polisi
 Wananchi  wa Ifuwa  Kilolo  wakiwatazama  viongozi  wao  wa kijiji  waliokamatwa na  polisi kwa agizo la  DC

 Wananchi  wa Ifuwa  wakiwatazama  viongozi  wao  wakiwa katika  gari la  polisi
 Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  akizungumza na  wananchi
 Mkuu  wa  polisi  wilaya ya  Kilolo  akizungumza na mmoja kati ya  viongozi  aliyekabidhiwa  vifaa vya  mwenyekiti  aliyekamatwa
 Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia  Abdalah  akizungunza na  wananchi  mara  baada ya  mkutano
Baba  mzazi wa Legani Msungu  akizungumza na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo baada ya  kuagiza  kijana  wake  akamatwe kwa  udalali wa  ardhi ,mzazi huyo  alimzawadia  zawadi  mkuu wa  wilaya kwa kazi nzuri  anayoifanya
 ...........................................................................................................................................................................


MKUU  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah  amewasimamisha  kazi  mwenyekiti wa    wa  serikali ya  kijiji cha  Ifuwa  kata ya  Idete  kupitia  chama cha mapinduzi (CCM)  Lasta Chavaligunga na  mwenyekiti wa  kitongoji cha mwagidawa Westen Nyamoga  kwa  tuhuma  za  kuuza  kinyemela  ardhi ya  kijiji  hicho  hekari zaidi ya  4000 kinyume na sheria ya  ardhi .


Pamoja na  kuwasimamisha kazi  viongozi hao amemwagiza  mkuu wa  polisi  wilaya ya  Kilolo  kuendelea  kuwashikilia  mahabusu hadi  ukweli  wa  tuhuma   hizo utakapojulikana na  wahusika  wengine kupatikana.

Mkuu   huyo  wa  wilaya  alichukua hatua  hiyo ya  kuwasimamisha kazi  viongozi hao juzi katika  mkutano wa  hadhara  uliofanyika  kijijini  hapo  ,mkutano   uliolenga  kushughulikia tuhuma  hizo za uuzaji wa ardhi  zilivyofanywa na  viongozi hao wa kijiji   hicho.

Akizungumza  katika  mkutano huo mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  kuwa   pamoja na jithada   kubwa zinazofanywa na  serikali ya  mkoa  wa Iringa  chini ya  mkuu wa  mkoa  Amina Masenza kwa  ajili ya  kuunga  mkono  jitihada za  rais Dkt  John Magufuli za  kusukuma  maendeleo kwa  wananchi  bado wapo  baadhi ya  viongozi wamekuwa  wakikwamisha  jitihada  hizo.

Kwani  alisema  utaratibu wa  uuzaji wa  ardhi  yenye  ukubwa wa  zaidi ya hekari  4000  hazimpi nafasi  mwenyekiti wa  kijiji ,  mkuu wa  wilaya ama mkuu  wa  mkoa kibali cha  kuuza  na mwenye mamlaka  ya  kutoa  kibali  ni  Rais wan chi  pekee  yake .

Aidha  alisema  kuwa  pamoja na ofisi yake   baada ya  kupata  taarifa  ya  uuzaji  wa ardhi  hiyo kumzuia  mwenyekiti  huyo   ikiwa ni  pamoja na kumweka  ndani  (mahabusu ) polisi  kwa  kukiuka  taratibu  za  uuzaji  ardhi bado mwenyekiti  huyo wa  kijiji alipotoka  aliendelea na mchakato wa kuuza ardhi ikiwa ni  pamoja na  kuchukua  pesa  kiasi cha  zaidi ya  shilingi 700,000 kwa  mwekezaji   huyo 

“ Huyu  mwenyekiti  wenu wa  kijiji  ni jipu amekuwa  akiendesha kijiji  kibabe  na  kutuuza  viongozi  wa  juu  hata mimi  amekuwa  akinipuuza nilishamweka ndani kwa haya  anayoyafanya  ila alipotoka  polisi  alikwenda  Dodoma na dalali  wake Legani Msungu na kwenda  kuchukua  pesa kiasi cha  shilingi 700,000”  alisema  mkuu  huyo wa  wilaya 

Kuwa  kutokana na mwenendo  wake  huo  wa  kuendelea  kufanya  ufisadi  wa  kuuza  ardhi ya  kijiji  kinyume na  taratibu  ameona  hafai  kuendelea  kuwa   kiongozi  katika  kijiji  hicho na badala  yake ataendelea   kuwa  mikononi  mwa  polisi  hadi uchunguzi wa  jambo   hilo  utakapokamalika  na   huyo  mwekezaji asikanyage  tena katika  kijiji  hicho.

Pamoja na   kumtaka  mwekezaji   huyo kutokanyaga katika  kijiji  hicho mkuu  huyo wa  wilaya  aliliagiza  jeshi la   polisi  wilaya ya  Kilolo  kumsaka  popote  alipo  dalali  wa mwekezaji huyo aliyemtaja kwa  jina la Legani Msungu  ambae ni mkazi wa  kijiji  hicho ili achukuliwe hatua kali .

Awali  mwenyekiti   huyo wa  kijiji akijieleza mbele ya  mkuu wa  wilaya alisema  kuwa kwa  upande wake hausiki na  uuzaji wa ardhi hiyo  isipo kuwa  familia  za wamiliki wa ardhi hiyo  ndio  ambao walikuwa  wakiuza na  yeye  alikuwa kama shahidi  upande wa  serikali .

Kufuatia  kutumbuliwa kwa  mwenyekiti huyo   wananchi  wa kijiji  hicho walimteua Matiasi Chahe   kuwa kaimu mwenyekiti wao .

Wakati  huo  huo  baba  mzazi wa  Legani Msungu  anayedaiwa  kuwani dalali  wa ardhi  hiyo  amempongeza  mkuu  huyo wa  wilaya ya  Kilolo kwa maamuzi yake .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE