April 14, 2018

CCM IRINGA MJINI KUENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI ,DIWANI CHADEMA APONGEZA

Machine za kufulia nguo na TV zilizotolewa na CCM Iringa mjini
Diwani wa Chadema kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi kushoto akimpongeza mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya kwa kazi nzuri za kusaidia maendeleo
Viongozi wa CCM na chadema Iringa mjini wakitazama chombo kilichokuwa kikitumika kufulia nguo hospitali ya Frelimo  kabla ya kukabidhi machine za kufulia nguo

WAKATI  diwani wa kata ya Mvinjeni kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema ) Frank Nyalusi akipongeza misaada mbali mbali inayotolewa na  chama cha mapiduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini  ,CCM wadai wataendelea kufanya kazi zilizo mshinda mbunge mchungaji Peter Msigwa .

Nyalusi alisema kuwa katika suala la maendeleo ni vema siasa kuweka kando na kuwa anapongeza jitihada za kimaendeleo zinazoendelea kufanywa na CCM Iringa mjini.

"Katika suala hili na maendeleo mnalolifanya CCM Iringa mjini hata Mimi nawapongeza sasa CCM haya ndio maendeleo ambayo wananchi wanataka"

Nyalusi alisema kuwa watanzania wakubali wasikubali Rais wa Tanzania ni Dkt John Magufuli na Meya wa Iringa ni Alex Kimbe huku mbunge wa Iringa mjini ni mchungaji Msigwa.

"Huu ndio ukweli lazima ifahamike kuwa viongozi waliochaguliwa ndio hawa tuwaheshimu na sasa tuache siasa chafu kwenye ukweli tuseme ukweli CCM Iringa mjini pamoja na kuwa Mimi ni chadema nawapongezeni sana"

Nyalusi alisema Nyalusi siasa za kuwekana mahabusu hazifai kwa sasa zifanyike siasa za kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya akizungumza leo na Radio Nuru Fm ya mkoani Iringa alisema kuwa wajibu wa CCM ni kuendelea kusaidia changamoto mbali mbali za wananchi wa jimbo la Iringa mjini ambazo mbunge wake Mchungaji Msigwa ameshindwa kuzitafutia ufumbuzi.

"Wajibu wa CCM ni kuwasaidia wananchi na tutaendelea kusaidia wananchi kwa kuzipa ufumbuzi kero mbali mbali"

Rubeya alisema walianza na kutekeleza ahadi ya TV katika soko kuu la Manispaa ya Iringa ,TV ambazo ziliahidiwa na mbunge Mchungaji Msigwa wakati wa kampeni na CCM kimefunga TV zaidi ya 4 katika soko hilo kama walivyoombwa na wafanyabiashara.

Pia alisema wamekabidhi mashine za kufulia nguo mbili na TV ya mafunzo kwenye Hospitali ya wilaya ,hospitali ya Frelimo na wataendelea kutekeleza kutatua kero mbali mbali za wananchi .

Mwenyekiti huyo alisema wajibu wa CCM ni kufanya kazi za kimaendeleo pasipo kuwabagua wananchi wa vyama vingine.
0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE