April 1, 2018

BREAKING NEWS:KKKT IRINGA WASITISHA KUSOMA WARAKAWARAKA


Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Blaston Gavile akitoka ibadani baada ya kumalizika ibada ya kwanza leo usharika wa kanisa kuu 
Kwaya kuu wakiimba ibada ya Pasaka 
Askofu Gavile akiwa na wachungaji na msaidizi wake mara baada ya kumalizika ibada ya Pasaka leo 

Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)  dayosisi ya Iringa Blaston Gavile leo amesitisha kusoma waraka wa maaskofu wa kanisa hilo kama ilivyopangwa kwa madai ya kuvuja kwa waraka huo.

Akitoa salamu za pasaka mara baada ya ibada ya kwanza katika usharika wa kanisa kuu leo, askofu Gavile alisema ilipangwa kusomwa waraka ila umesitishwa kusomwa baada ya kuvuja hivyo anayehitaji kusoma waraka huo wa kitume afike ofisini auchukue ila hautasomwa tena kanisani. 


Habari kamili itakujia au tembelea chanel ya Youtube Matukiodaima zaidi soma gazeti la mtanzania kesho jumatatu

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE