April 4, 2018

ABDUL NONDO LEO MAHAKAMANI DAR

TAARIFA KUHUSU KESI YA  ABDUL NONDO
Leo tarehe 4 April 2018, Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imeendelea kusikiliza kesi ya Mwanafunzi na mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo. 

Katika kesi hiyo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na TSNP ililazimika kupeleka maombi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kumshtaki Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuiomba Mahakama iamuru vyombo husika kutoa dhamana kwa bwana Nondo, kumpeleka Mahakamani ili aweze kusikilizwa au kumwachia huru.

 Maombi hayo  ya Jinai Namba 49 ya mwaka  2018 yamesikilizwa leo tarehe 21/3/2018 mbele ya Jaji Rehema Sameji.

Katika kesi hiyo Mahakama ilitaka kutupilia mbali maombi ya wapeleka maombi kwani tayari kesi ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa, na hivyo Mahakama Kuu kukosa mamlaka ya kuendelea na kesi hiyo. 

Hata hivyo Wakili wa upande wa wapeleka maombi, Wakili Mpoki aliiomba mahakama iendelee na itoe uamuzi kuhusu maombi yaliyoletwa huku akionesha umuhimu wa Mahakama kutoa uamuzi kuhusu maombi hayo. 

Baada ya kusikiliza maombi wakili wa upande wa wapeleka maombi, Mahakama imeamuru pande zote zifike mahakamani tarehe 11/04/2018 kwa ajili ya kusikilizwa hoja zao na baadae itatoa uamuzi.

*Imetolewa leo tarehe 05 April, 2018*
*Na:*
*THRDC*

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE