March 28, 2018

WAWILI WAJINYONGA IRINGA AKIWEMO RAIA WA INDIA....

RPC IRINGA JUMA BWIRE
..............................................
WATU  wawili  wamejiua kwa  kujinyonga  kwa  kamba  mkoani  Iringa akiwemo mmoja  mwenye  asili  ya kihindi aliyejinyonga baada ya mkewe kusafiri kwenda  nchini  kwao India.

Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Juma  Bwire  ameueleza mtandao wa matukiodaima  kuwa  matukio hayo mawili  yametokea  kwa  nyakati  tofauti katika    kijiji cha  Tagamenda  kata ya  Luota  wilaya ya  Iringa  vijijini  kwa  mkazi  wa  kijiji  hicho Waziri Nzengere (43)  mkulima  wa  kijiji  hicho  alikutwa  akiwa amejinyonga  kwa   kutumia  kamba ya manila  kwa  kuifunga  kwenye  mti katika  shamba lake.

Kwa  mujibu wa kamanda  Bwire  alisema  tukio hilo  Machi 26 mwaka  huu  baada ya  ndugu  wa marehemu  huyo  aliyejitambulisha kwa  jina la Alphonce Nzegere  kutoa  taarifa  polisi  kuhusiana na kifo  cha  mtoto  wake   huyo.

Kamanda  huyo  alisema  baada  ya uchunguzi wa madaktari  walibaini  kuwa  kifo chake  kimetokana na  kujinyonga na  mwili  umekabidhiwa kwa  ndugu kwa  ajili ya mazishi  baada ya  ndugu  kutokuwa na  hofu  juu ya kifo  hicho.

Aidha  katika  tukio la  pili kamanda  Bwire  alisema   machi 26 majira ya  mchana polisi walipewa  taarifa  ya  kifo  cha   Hiren Shantilal  Makvana  (29)   mwenye  asili ya  kihindi  aliyekuwa  akifanya kazi katika  ofisi ya Electronic Techical - Aitel Iringa  na  kuishi katika eneo la Gangilonga mjini hapa.

Kuwa Hiren alikutwa amejinyonga  katika  chumba  chake  alichopanga  kwenye  jengo la  NSSF  kata ya  Gangilonga  kwa kujifunga nguo shingano na  kisha  kuifunga katika feni aina ya Panga Boy  iliyopo ndani ya  chumba chake .

Alisema  kuwa mke  wa marehemu  huyo  alikuwa amesafiri  siku za  nyumba kwenda nchini India  na  kuwa marehemu  hakuacha  ujumbe  wowote juu ya  hatua  yake  ya  kujinyonga

Habari za mitaani ambazo matukiodaima imezipata ni kwamba mhindi huyo alitakiwa kuondoka kwenda India ndani ya mwezi ujao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE