March 21, 2018

WASHIRIKI ZAIDI YA 50 WAKIWEMO 6 KUTOKA NCHI MBALI MBALI WASHIRIKI MAONYESHO YA KIBIASHARA YA ZANA ZA MAZAO YA MISITU NA MBAO IRINGA

mkufunzi  wa  chuo cha viwanda  vya misitu  - FITI Moshi  Bw Cuthbet Naburi akitoa  elimu ya msumeno  wa  kuchania mbao  kutoka kampuni ya Slidetec wakati  wa maonyesho ya kibiashara  ya zana za misitu na mbao wilayani Mufindi  mkoani Iringa
Mshiriki wa maonyesho ya  kibiashara  ya zana za  mazao ya misitu na mbao kutoka kampuni ya kimataifa ya  Wood -Mizer wakionyesha  mashine ya  kisasa  ya uchanaji mbao kwa  haraka  zaidi
Wakulima wa miti wilayani  Mufindi  walionufaika na Programu ya Panda Miti kibiashara kutoka vikundi  vya  kifedha mbali  mbali wakipata maelekezo ya mashine ya  uchanaji  mbao  kutoka kampuini ya Slidetec 
......................................................................................
                      Na Matukio daimaBlog
ZAIDI  ya waonyeshaji  wa 50   yakiwemo makampuni 6 kutoka nje ya Tanzania wamejitokeza kushiriki  katika maonyesho  ya   zana  za  kisasa za kibiashara  ya mazao ya  misitu na mbao   katika  mikoa ya nyanda  za  juu  kusini .

Katika  maonyesho hayo ya siku  mbili  yaliyofanyika  katika viwanja vya  ofisi ya   Programu ya panda  miti  kibiashara  ( Privete Forest Programu (PFP) mjini Mafinga wilayani  Mufindi mkoani Irina kwa  kuwashirikisha  wakuu wa  mikoa ya  Iringa  , Njombe ,Mbeya  na Songwe  wadau  wa   PFP  walipata  fursa  ya kunufaika na maonyesho  hayo   kwa kuonyeshwa  mashine  za kisasa  za  bei  nafuu  za uchanaji mbao .

Mbobezi  katika  fani ya  misitu Dkt Felician Kilahama ambae  ni  mwenyekiti  wa  bodi ya taasisi ya utafiti  wa misitu Tanzania  (TAFORI) akizungumza  katika  mahojiano  maalumu na mwandishi wa  habari  hizi kwenye maonyesho  hayo  alisema  kuwa  maonyesho  hayo  ni ukombozi  mkubwa  kwa   wadau  wa  misitu na mstakabari  wa  serikali  ya  awamu ya  tano   chini ya  Rais Dkt  John Mafuguli ambayo  imeweka  mkakati  wa kuelekea  serikali ya  viwanda .

Alisema  kupitia maonyesho  hayo ni fursa  kubwa kwa  wananchi kujiongeza kwa  kujikita katika kilimo  cha mazao ya  miti na  hata  kuingia  katika teknolijio  ya  kisasa ya matumizi  ya  mashine za kisasa  za  kuchana  mbao na kuongeza uzalishaji wenye  tija wa  mazao ya  miti  kwa faida  zaidi .

“ Hii  ni fursa nzuri  kwa misitu  kuweza kuchangia ukuaji  wa   sekta ya  viwanda  na watu hawawezi  kuingia  katika  uwekezaji wa  sekta  ya viwanda  vya  misitu  bila  kujua faida  yake  kwa  sababu  kinachofanyika katika  maonyesho haya  hapa Mufindi  mkoani  Iringa ni  kuwafunuamacho kuweza  kujua  ni  namna gani  wanaweza  kuanzisha  viwanda  vyao  kupitia sekta  hii ya misitu na katika  misitu  kuna  fursa  zipi  za  kiuchumi  na mimi  nilitamani  jambo hili lingefanyika  wakati  ule  nikiwa mkurugenzi wa misitu na nyuki  lakini  halikuweza  kufanikiwa  ila  niwashukuru  hawa  wenzangu wa  Panda  miti  kibiashara wametimiza ndoto  yangu  “
Alisema  kuwa imani yake  kubwa kupitia  program  hiyo iliyopo chini ya  serikali  ya  Tanzania  kwa  ufadhili  wa  nchini ya  Finland   iwapo  wananchi  wengi  wakajikita katika upandaji  miti  uchumi na  uanzishaji  wa  viwanda  vya mazao ya  misitu  uchumi wa nchi  utakua  zaidi  na kila  mmoja atanufaika na  programu ya  panda  miti  kibiashara ambayo nimkombozi  mkubwa kwa  mwananchi hapa  nchini kwa  misitu ni uchumi  endelevu .
Dkt  Kilahama  alisema  kuwa  zana  ambazo  zimeonyeshwa  katika  maonyesho   hayo  kwa  wakulima  wa  mazao ya  misitu na  mavunaji  ni  zana ambazo  ni  za  kisasa  na  zinapunguza upotevu  mkubwa  uliokuwepo kwa  wavunaji ambao  walikuwa  wakitumia zana zisizo  za  kisasa  kuvuna mazao ya  misitu .
“Mvunaji  awali kabla ya mashine  hizi  zilizoletwa  kwenye  maonyesho  haya  akitumia  mashine  za awali katika  gogo  moja alikuwa akipata  asilimia 37 hadi  40  au  pungufu ila  sasa  atapata asilimia 50  hadi  99 na zaidi  hivyo  huu  ni  ukombozi  mkubwa na kweli  serikali  itaweza  kupata  mapato  yake  na  jambo hili liwe  endelevu  zaidi  “

Katika  hatua  nyingine  Dkt  Kilahama  alishauri  kuwa  kutokana na  maonyesho hayo  ya  zana  za  kibiashara  za  mazao ya  misitu na mbao  kuwepo  kwa mkakati  endelevu  utakaoepesha  Taifa  kutumia samani kutoka  nje ya  nchi  nabadala yake magogo na mbao  kutumika kutengeneza  samanihapa nchini na  kuuza samani  nchi  na kuepuka  kununua  samani  kutoka nje ya  nchi  ili  kuongeza uchumi wa nchi .

 Japo  alisema  zipo  sheria  zinazozuia  magogo  kusafirishwa  nje  ya  nchi  isipo  kuwa   mbao  japo  alitaka hata  mbao  zisirusiwe  kutoka  Tanzania  ila samani  zirusiwe  baada ya  kutengenezwa  hapa nchini  kwa  ubora  mzuri .

Akifungua  maonyesho  hayo  mkuu  wa mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza pamoja na  kuwapongeza  wakuu wa  mikoa ya  Njombe ,  Ruvuma , Mbeya na  Songwe  kwa  kushiriki   katika  maonyesho hayo na  kuunga  mkono programu ya  Panda  Miti  kibiashara  bado  alishauri  maofisa misitu  wa Halmashauri  zote  za mikoa  husika  kuja na  mpango mkakati  wa  kuwezesha  wananchi  kunufaika na mpango  huo  wa upandaji  miti kibiashara .

“ Napenda  kuwashukuru wizara ya  maliasili na utalii kupitia  mradi  wa   panda miti  kibiashara  kwa  maandalizi  haya  mazuri  ya  maonyesho  haya  mradi  huu wa panda  miti  kibiashara ni mradi  wa  serikali ya  Tanzania  uliofadhiliwa  kwa  pamoja na serikali ya Finland na Tanzania kupitia  wizara ya  maliasili na utalii  napenda  kuwashukuru  walipa kodi la  Finland  kwa msaada  wao  huu “

Hivyo  aliwataka  wananchi wa  mikoa iliyolengwa na mradi  huo kutumia  nafasi  hiyo kujiunga katika  mnyororo  wa  kujikwamua  kiuchumi kwa  kupanda  miti kibiashara huku  akiwataka  wale  wote ambao  bado  kujiunga katika mradi  huo  kujitokeza na  kujiunga .

Mshauri  wa  kitaifa  wa  misitu katika  program  ya  panda miti  kibiashara  ambae  ni bwana  miti pia Sangito  Sumari   alisema  kuwa lengo la  maonyesho  hayo ni  kuwaunganisha pamoja  wajasiliamali  waliojikita katika  sekta  ya  misitu na  kuwaonyesha  fursa  za  ukombozi  kwao  kwa  kuwaonyesha  taasisi za kifedha  ambazo  zinaweza  kuwasaidia.

Alisema katika  maonyesho  hayo  taasisi  zaidi 40  ambazo  zimeshiriki kutoka ndani ya  nchi ambazo nitaasisi  kubwa na ndogo   na  watu  binafsi pia  wawakilishi wa mashirika 6   duniani  yamepata  kushiriki  maonyesho  hayo  ambayo ni  China , Finland , India  ,Afrika  Kusini  na  nchi  nyingine  marafiki  ambao  wanajihusisha na  shughuli za  mazao ya  misitu .

Alisema  kuwa  mradi  huo ambao  unatoa  huduma  zake  bure  kwa kutoa  miche  na  ushauri  kwa  wakulima  wa miti  unafanya kazi  katika mikoa ya  Iringa kwa wilaya ya  Kilolo  na Mufindi , Njombe kwa wilaya ya Makete , Ludewa na  Njombe   , Morogoro kwa wilaya ya  Ulanga na Kilombero ,Ruvuma ni wilaya ya   Songea  vijijini  na Nyasa  na  Mbinga  .

Alisema  katika  mikoa ya  wilaya tajwa wamekwisha  pata  misaa mingi kwa vijiji zaidi ya 100  ambavyo  vimepewa misaada  mbali mbali  ya  ruzuku  katika shughuli yaupandaji  miti  na ujasiliamali  nanyingine.
Kuwa  mradi  huo  umeanza  toka  mwaka 2014  na kwa  sasa  mradi  huo  umeongezwa  muda  wa mwaka  mmoja  baada ya  serikali  kuona  ni mradi  mkombozi wa wananchi hasa  katika  sekta ya  misitu na utaisha  Desemba  2018  na  awamu ya pili itakuwa miaka  mitano  mingine .

Miongoni  mwa  waonyeshaji  wa zana za kisasa za mazao ya misitu na  mbao walioshiriki  ni  pamoja na  Sao hill Mufindi ,Saw Specialists (Pty) Ltd  kutoka Afrika  ya  kusini ,STIHL kutoka Dar es Salaam ,chuo cha chuo cha viwanda  vya misitu  - FITI Moshi ,Propramu ya Panda  miti  kibiashara ambao  ndio waratibu wa maonyesho hayo,Mkaa endelevu kutokaa Mufindi,Slidetec kutoka nchini Finland na  wengine wengi.
TAZAMA  VIDEO  MBALI  MBALI  HAPA  CHINI 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE