March 8, 2018

UTATA WAIBUKA KUTEKWA KWA MWANAFUNZI

Nimepata Taarifa ya mshangao mkubwa jioni ya leo punde tu nilivyowasili nyumbani kwangu Mafinga jioni ya leo baada ya kuona kwenye mitandao ya kijamii na kusikiliza kwenye vyombo vya Habari sasa nakaa natafakari ni aina gani ya vijana tuliokuwa nao

Mapema leo asubuhi muda wa saa 12:00 asubuhi nilipanda gari aina ya NEW FORCE yenye  namba ya usajili ya T 226 DJQ  nakukaa siti yenye namba G3 ambapo jirani wangu aliyekuwa amejivika shuka la kimasai alikuwa amekaa siti namba G4 ambaye alionekana kuwa na hofu wakati wote na kutumia simu yake kwa kutuma jumbe tofauti kila mara

Wakati tupo njiani kijana yule nilitaka kujenga urafiki walau Tupige hata stori mbili tatu lakini ilishindikana ila tulipofika Morogoro ndipo alianza kunisemesha kwa kuhitaji nimsaidie kununua maji kwa kuwa nilikuwa upande wa dirishani nikafanya hivyo nikiwa na dhamira ya kumsaidia ndipo tulipoanza kupiga stori mbili tatu

Lakini nilisikia tukiwa njiani anawasiliana na mtu mmoja mwenye sauti ya kike na kumtaka aandae mazingira ya hapo wanapokutani.

Wakati wote namuaangalia kijana huyu ambaye awali nilikuwa simfahamu vizuri nilimbaini kwa sura nikamjua na hakutaka kuongea na mimi zaidii ya kujifichaficha

Sasa nimefika nyumbani Naanda kusikiliza radio nasikia kuna kijana wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kutekwa nilipoingia Facebook ndo nikaona picha yake nikamwambia mke wangu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kuwa kijana huyu nimependa naye basi moja kutoka Dar es Salaam na mke wangu hakuamini

Nipende kuambia ndugu watanzania wenzangu kijana huyu HAJATEKWA WALA NINI MAANA NILIKUWA NAYE MWANZO WA SAFARI YOTE NA KAMA KATEKWA LABDA NI KWENYE NDOTO

HIVYO TAARIFA ZOTE ZA UTEKWAJI WAKE NI ZA KUPUUZWA MAANA ANATAKA KUTAFUTA UMAARUFU WA AJABU KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII

JONATHANA KWEPE


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE