March 9, 2018

UNDANI WA HABARI YA MWANAFUNZI ALIYETEKWA ALIVYOFIKISHWA KWA RPC

BAADA  ya  mwanafunzi  wa  mwaka  wa tatu  kitivo  cha  siasa  na utawala  chuo  kikuu cha  Dar es Salaam  Abdul  Nondo  ( 24) ambae  ni  mwenyekiti  wa  mtandao  wa wanafunzi  Tanzania (TSNP)kudaiwa   kutekwa na  watu  wasiojulikana , jeshi la  polisi limemwonyesha  mwanafunzi  huyo  mbele ya  wanahabari na kuahidi  kuchukua hatua za  kisheria iwapo  itabainika  katoa  taarifa  za  uongo  .
 
Mwanachuo  huyo  ambae  aliletwa  jana majira ya  saa 4.45  asubuhi makao  makuu ya  polisi mkoa  wa Iringa akiwa  katika  gari dogo  binafsi   aina ya  Toyota  Porte lenye namba  za  usajili  T 256 DDW  akiwa  chini ya  ulinzi wa   maofisa wa  polisi   watatu  akitokea  kituo  cha  polisi Mafinga wilayani  Mufindi  .
 
Akizungunza  na  matukiodaimablog na TV  kuhusiana na  mwanafunzi huyo kamanda wa   polisi  mkoa wa  Iringa  Juma Bwire  alisema  kuwa  mwanafunzi  huyo  ambaye  alisemekana amepotea  katika mazingira ya  kutatanisha  mkoani  Dar es  Salaam  alipatikana  Machi  7 mwaka huu majira ya  saa 1  asubuhi  Nondo  alifika katika  kituo  kidogo  cha  polisi Mafinga   wilaya ya  Mufindi  na kueleza  kuwa alitekwa na  watu wasiojulikana.
 
  Jeshi la  polisi  mkoa   wa Iringa limefungua  jalada la uchunguzi  ili  kubaini  ukweli  kama  alikuwa ametekwa  na  kama kweli alikuwa ametekwa  tunaahidi  kwamba  sisi jeshi la  polisi  tukipata ukweli watuhumiwa wote  sheria  itachukua  mkondo  wake “
 
Aidha alisema  jeshi la  polisi linaendelea na uchunguzi  kama  atakuwa  ametoa  taarifa  za  uongo  kwa  nia ovu kwa lengo la  kutaka  kuhamasisha wanafunzi wenzake  ili  kuleta uvunjifu wa amani nchini  watamshughulikia  kama  wahalifu  wengine  .
“ Kwa  sasa anaonekana hali yake   ni  nzuri hana majeraha ,makovu  na afya  yake  ni  nzuri kama  mnavyo  muona hapa mbele   yenu “
 
Kamanda  Bwire  bila  kutaka  mwanafunzi  huyo  kuulizwa  maswali na  wanahabari ama yeye  kuulizwa maswali kwa  sasa alisema  asingehitaji  maswali kwake  wala  mwanafunzi  huyo kutokana na  sababu   kutovuruga uchunguzi  wa  tukio  hilo .
 
Huku akiwaomba  wananchi  wenye taarifa  zozote  zinazohusiana na  mwanafunzi  Nondo  kujitokeza kutoa  ushirikiano  ili  kukamilisha  uchunguzi  wa  tukio hilo na  kuwa  jeshi la polisi linaendelea  kumhoji  zaidi  mwanafunzi  huyo.

Katika   jumbe  mbali mbali  za kwenye  mitandao ya kijamii  iliyoripoti  juu ya   tukio hilo mara ya  mwisho  kabla y a jitihada za  wanaharakati kuanza kumtafuta   Nondo  kwa  kuripoti  kituo kikuu  cha polisi jijini  Dar es  Salaam  na  kupewa  RB namba ; UD/RB/1438/2018  walishitushwa na ujumbe uliotumwa na Nondo  kupitia  simu yake ya  kiganjani  uliosomeka   Iam at High Risk ujumbe  uliokuwa na maana ya kuwa  niko hatarini  .

Kufuatia  ujumbe  huo  simu ya Nondo  haikuweza kupatikana  tena  hivyo kufuatia  kuwa  Ndondo ni  mmoja kati ya  watetezi wa  haki za binadamu  akihusika  zaidi kutetea haki za  wanafunzi  wa vyuo  vikuu tofauti  nchini  ,mtandao wa  watetezi wa haki za  binadamu  (THRDC ) kama  chombo  kinachotetea  haki za  binadamu  ulisimama  mbele  kuendelea  kumtafuta  mtetezi  huyo kabla ya  kupatikana  juzi asubuhi akiwa mjini Mafinga  na kwenda kituo cha  polisi  kutoa taarifa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE