March 29, 2018

SUMATRA YAJA NA SHERIA MPYA ITAKAYOZUIA BIASHARA NA MAHUBIRI NDANI YA MABASI ,RC IRINGA AONYA MADEREVA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akifungua warsha ya pamoja ya watoa Huduma za usafirishaji Mkoa wa Iringa Leo 
Viongozi mbali mbali wakiingia katika ukumbi wa siasa ni kilimo leo
Afisa wa Sumatra Mkoa wa Iringa Pateli Ngereza akieleza lengo la warsha hiyo
Mwanasheria wa Sumatra Mwadawa Sultan akitoa elimu ya sheria mpya za Sumatra leo

MAMLAKA ya usafirishaji majini na nchi kavu ( Sumatra) imejipanga kuja na sheria mpya itakayopiga marufuku wafanyabiashara na wahubiri kutofanya shughuli hizo katika mabasi.

Mwanasheria wa Sumatra Makao makuu Mwadawa Sultan ameyasema hayo leo katika ukumbi wa siasa ni kilimo wakati wa warsha ya watoa Huduma wa vyombo vya usafiri mkoani Iringa.

Alisema lengo la kuja na sheria hiyo ni kuepusha usumbufu kwa abiria wawapo safarini .

Kwani alisema imekuwa ni kawaida kwa watoa Huduma hao has a wahubiri ama wafanyabiashara kuzunguka katika mabasi kufanya Huduma zao kinyume na sheria za utoaji wa Huduma hiyo.

"Tutaanza kuchukua hatua Kali kwa wahubiri hao na wafanyabiashara pamoja na wa Huduma wa vyombo vya usafiri vitakavyo kiuka"

Alisema kuwa kupitia sheria mpya kuanzia sasa ni marufuku Huduma hiyo kutolewa katika vyombo vya usafiri.

Kwa upande wake afisa wa Sumatra Mkoa wa Iringa Pateli Ngereza alisema kuwa pamoja na mafanikio mbali mbali ya uboreshaji wa Huduma za usafiri ila ipo changamoto ya ongezeko la nauli kutokana na kupanda kwa bei za Mafuta.

Alisema katika Mkoa wa Iringa kumekuwepo na ushirikiano mkubwa kwa wananchi kutoa ushirikiano japo badhi ya maeneo ya mji wa Iringa changamoto ya miundo mbinu ni kubwa.

Aidha alitaka wafanyabiashara kuendelea kuagiza magari yanayobeba abiria wengi zaidi na kuanzia sasa hawatatoa leseni ya njia kwa magari madogo.

Hivyo alishauri wafanyabiashara kuungana ili kuagiza magari makubwa kama kampuni.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alitaka magari ya abiria kuwa na bima kubwa ili pindi ajali zinapotokea kuwalipa Fidia wahanga kwa wakati.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE