March 30, 2018

SHIRIKA LA RDO LAMWAGA MAMILIONI YA PESA KUTATUA KERO YA MAJI


Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza wa pili  kushoto akiwa na mkurugenzi wa RDO Fidelis Filipatali akimwelezea  jambo
Mkuu wa  mkoa wa Iringa  na  viongozi mbali mbali  wakitembelea  mradi wa maji wa RDO
Mkurugenzi RDO kushoto  akimweleza jambo mkuu wa mkoa wa Iringa
Mkuu wa wilaya ya  Mufindi  Jamhuri  Wiliam kushoto  na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na mkurugenzi RDO wakitazama mradi wamaji
wananchi  wakiwa katika maadhimisho hayo
SHIRIKA  la maendeleo  vijijini (RDO) limetumia  kiasi cha shilingi  milioni 93,503,100 kuwajengea mradi  wa maji  wa  bomba wakazi wa kijiji cha Nandala kata  ya Ihanu  wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa .

Mratibu wa mradi  huo  wa maji – Wata unaofadhiliwqa na RDO Fidelis Filipatali  alisema  juzi  wakati wa kilele  cha maji  kwa mkoawa Iringa  kuwa fedha  hizo  zimetolewa na  wafadhili wa RDO ambao wamechangia  zaidi ya shilingi  milioni 86.6 na  mchango  wa  wananchi  ni  milioni 8,682,100.

Alisema  mradi wa RDO  wamefanikiwa  kwa  kiasi kikubwa  kushirikiana na  Halmashauri ya  wilaya  ya Mufindi  katika  uendelezaji  wa  upanuzi  wa mradi  wamaji safi  na salama  katika  kijiji  cha Nandala  na vijiji vingine  vya  wilaya ya Mufindi  na  Kilolo .

Filipatali alisema  shughuli  za usimamizi wa  miradi hiyo  zimekuwa  zikifanywa kwa ushirikiano  mkubwa  wa  serikali  za  vijiji  husika  na  miradi  hiyo  husimamiwa  na  wananchi  wenyewe  kupitia  jumuiya  za  watumiaji maji .

Akielezea  changamoto zinazokabili  miradi  hiyo  kuwa ni kutowajibika  ipasavyo  kwa baadhi ya  watumiaji maji  kutotimiza wajibu wao pamoja na  baadhi ya  wanasiasa   kutumia  miradi hiyo  kujitafutia  umaarufu  wa  kisiasa .

Aidha  aliishauri  serikali  kupitia  mamalaka ya mapato  Tanzania (TRA)  kutoa kodi  kwenye manunuzi ya malighafi  za maji ilikuwafikia  watumiaji  wengi  zaidi ,pia  kupunguza urasimu  wa  vitengo  vingi  kwenye idara  ya maji ambavyo  vipo katika  njia ya  kupunguzamchakato  mrefu  wa  shughuli  mbali mbali kama  upatikanaji wa  vibali .
Aidha  kutoa hati  za  Trustee katika  miradi  inayotoa huduma   sehemu  kubwa ili  kuepusha  mgangano  wa  kikatiba  kwa  watumiaji maji wa  vijijini .

Mratibu huyo  alisema  kwa  sasa RDO  imejipanga kuendeleza upanuzi wa miradi ya maji katika  vijiji  vya Mkonge , Isipii ,Lulanda  na  baadhi ya  vitongoji  ambavyo  vilikuwa havina huduma  ya  maji kwenye  wilaya ya  Mufindi na  kuwa  upanuzi  huo  utaihusu  wilaya ya  Kilolo .       

Awali  akitoa  risala ya  watumiaji  maji wa kijiji  cha Nandala  Malkia Kangalawe   alisema kuwa  mradi  huo  ulianza  kujengwa  mwaka 2016 hadi mwaka 2017 kuwa  mradi huo ni  moja kati ya  miradi  inayofadhiliwa na RDO  na  kuwa jumla ya  wananchi 1038 na taasisi  mbili  zitanufaika na mradi  huo wa maji .

Kwa  mujibu wa mhandisi wa maji  mkoa  wa Iringa Shaban  Jellan wananchi  wa  mkoa wa Iringa  wanaopata  huduma ya maji  safi na  salama ni  asilimia 71.2 kwa  wakazi 941,238 kwa  mujibu wa  senza ya  watu na makazi  ya mwaka 2012.
Huku kwa upande wamamlaka ya maji  safi na  usafi wa mazingira  mjini Iringa (IRUWASA) hali  ya utoaji wa  huduma  ya maji  safi   imefikia asilimia 96 na majitaka ni  asilimia 17 .

Kuwa  mkoa wa Iringa  ulipanga  kujengha jumla ya  miradi 33 vijijini  kupitia program ya  maendeleo ya sekta ya maji  kuanzia  mwaka 2006/2007 ila hadi  kufikia Februari 2018 jumla ya  miradi  21 katika  vijiji 24 imekamilika  na miradi 12 iliyobaki  iko katika  hatua mbali mbali za  ujenzi na  mkoa umebakia na kiasi cha shilingi  milioni 750 kutoka  wizara ya maji  na umwagiliaji kwa ajili ya  kuwalipa  wakandarasi wa miradi hiyo .

Kwa upande wake  mkuu wa mkoa wa Iringa mbali ya  kuwaonya  wafadhili  ambao wameingia katika  miradi hiyo kwa ajili ya  kufanya  siasa  za  kuichafua  serikali ukiwemo mradi wa Water for Africa ambao  umeanzishwa na mbunge  wa  jimbo la Mufindi kusini ila  wafadhili  wake  wanapandikiza  chuki dhidi ya  Rais kuwataka  kuondoka nchini .

Bado  alisema  baadhi ya  taasisi kama  RDO  zimekuwa  zikifanya  vizuri katika utoaji huduma kwa  wananchi na  uendeshaji wa  miradi  bila  kuingiza  siasa chafu .

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati na kutambua mchango unatolewa na wadau mbalimbali ikiemo RDO, PDF, WARIDI, IECA, UNICEF, Water for Africa na taasisi za Dini katika kuwatua akina mama ndoo kichwani kupitia ujenzi wa miradi ya maji katika Kata ya Mdaburo Nashauri Wakurugenzi kutoa msaada na ushirikiano wa hali na mali kwa mfadhili huyu pamoja na wafadhili wengine ambao kwa kiasi kikubwa mchango wao unaongeza upatikanaj wa maji katika Mkoa wetu wa Iringa ila  sitaki miradi  hii  itumike kisiasa “

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE