March 26, 2018

SABABU ZILIZOSABABISHA JOKATE MWEGELO KUTIMULIWA UVCCM

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi jumuiya hiyo, Jokate Mwegelo ni maazimio yaliyoridhiwa na Baraza Kuu la Jumuiya hiyo.
Uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi huo wa Jokate, umetangazwa leo na Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James mjini Dodoma leo Jumapili Machi 25, Kufunga Kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo, iliyotanguliwa na semina elekezi huku akisisitiza nafasi hiyo itajazwa baadaye.
Akizungumza na Mtanzania Digital, Shaka amesema sababu za kutenguliwa kwa Jokate inatokana na uamuzi wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo iliyokutana kwa dharura leo mchana chini ya Mwenyekiti wake, Kheri na kuazimia kwa pamoja ambapo hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida wa vikao vya baraza hilo ambapo ajenda inapowasilishwa bila kujali aliyewasilisha ni nani na kikao kinaporidhia inakuwa ni ajenda ya kikao.
“Itoshe tu kusema ni utaratibu wa kawaida ndani ya CCM pamoja na jumuiya zake kufanya mabadiliko ya aina yoyote pale wanapoona inafaa,” amesema shaka kwa kifupi.
Jokate ametumikia nafasi hiyo kwa miezi 11 tangu ateuliwe Aprili 24, mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE