March 31, 2018

TUMEJIPANGA KWA ULINZI IRINGA PASAKA OLE WAKE ATAKAYEVURUGA AMANI -RPC BWIRE

 kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire 
......................................................................................................................................
                                   Na MatukiodaimaBlog

Alisema  kuwa nyumba  zote za ibada  kwa  siku ya leo  jumapili  wakati waumini  wa  dini ya  kikristo nchini  wakiungana na wenzao  ulimwenguni  kusherekea   sikukuu ya  kumbukumbu ya  kufufuka kwa Yesu Kristo  sikuu ya  Pasaka  zimewekewa  ulinzi na hakuna  mharifu ambae ataingia katika nyumba yeyote ya  ibada  kufanya uharifu .

Kamanda  huyo  alisema  pamoja na kuweka  ulinzi katika  nyumba  za ibada  bado amewataka  waumini na  viongozi wa makanisa  kuhakikisha  wanakuwa makini na  kuwaelimisha  waumini  wao kutoacha vitu ovyo na  kutuwaamini  wageni  ambao watafika kuabudu katika  nyumba   hizo za ibada kwani  kupitia  sikukuu hizi ni rahisi  waharifu kujipenyeza miongoni mwa waumini  kwa lengo la  kuwaibia pochi  ama simu zao .

Alisema  pia  jeshi  hilo  limeweka  ulinzi katika maeneo mbali mbali ya  starehe  ,mitaani na barabarani  kuona  hakuna madhara  yeyote  yatakayojitokeza  ya uharifu ama ajali  katika  kipindi  hiki cha  sikukuu .

" Leo  tunafanya  ulinzi mkali katika maeneo yote kuona  wananchi  wanasherekea  sikukuu kwa amani na utuluivu  zaidi  ulinzi wetu na  wa askari wa magari ,pikipiki ,askari wa  miguu na askari ambao watakuwa  kiraia ambao  wafanya kazi ya  kulinda  usalama  sasa  ole  wako wewe  ambae utajipenyeza katika  eneo  moja  wao  kuvuruga  amani utakiona"

Pia  alisema   jeshi hilo  litawachukulia  hatua kali  wale wote watakaofanya  biashara ya  Disco toto bila kibali na kama kuna  kibali basi wazingatie vibali vyao kwani iwapo watakiuka ama kufanya pasipo  ruksa sheria  itachukua mkondo  wake.

"Kwa  kawaida  vibali  vya disco ama  burudani hutolewa na maofisa  utamaduni na  sisi jeshi la  polisi  tunapewa taarifa pamoja na kuvipitisha  ila  disco toto  kwa kawaida  huwa mchana na hufanyika sehemu  salama itakayozingatia usalama wa  watoto  hao "

Kuhusu madereva kamanda  huyo aliwataka  kujiepusha na ulevi wakiwa katika  vyombo  vya  moto na  kuwa dereva ambaye  atakutwa  akipiga honi  ovyo atakamatwa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE