March 6, 2018

RPC MPYA IRINGA AELEZA UTEKELEZAJI WA AGIZO WA OPARESHENI YA WIKI MBILI ,WAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 83 KWA WIKI MBILI

Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa  Iringa Juma Bwire Makanya - ACP akizungumza na wanahabari   juu ya  Oparesheni  iliyofanyika
 KAMANDA  wa  polisi  mkoa  wa  Iringa Juma  Bwire Makanya  asema  ametekeleza agizo  la  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  na  kufanya  oparesheni ya  vyombo  vya  moto vibovu ndani ya  wiki mbili  alizopewa  kwa kuiingizia  serikali kiasi cha shilingi 83,160,000 .

Akizungumza na  mtandao  wa matukiodaimaBlog na TV   ofisini  kwake jana  Kamanda  Makanya   alisema alipewa  muda wa  wiki  mbili wakati wa  uzinduzi wa  wiki  ya  nenda  kwa  usalama  barabara  agizo  lililotolewa na  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  aliyemwakilisha  mkuu wa  mkoa katika maadhimisho  hayo .

"  Kama  mtakumbuka  wakati  wa  maadhimisho  hayo mgeni  rasmi  aliliagiza  jeshi la  polisi  kufanya  oparesheni kali ya vyombo  vya  moto  vibovu na ile ya  kusaka  waharifu  tumetekeleza  kwa  muda  tuliopewa "


Alisema  katika  oparesheni   hiyo  iliyoanza Februari 15  mwaka  huu hadi Machi 1  askari  wa  usalama  barabarani   wamefanikiwa  kukamata jumla ya makosa  2,842 kwa  kukamata  magari 2,430 , bajaji 94 na  pikipiki 318 .
Kamanda  Makanya   alisema  kupitia  oparesheni  hiyo  ya  wiki  mbili  jeshi la  polisi  mkoa wa Iringa  limefanikiwa  kuiingizia  serikali  kiasi cha  shilingi 83,160,000 kutokana na faini  mbali mbali  zilizotozwa .


Hata  hivyo pamoja na  kutekeleza  agizo hilo kwa  wiki mbili kama  walivyopewa  bado oparesheni ya vyombo  vya  moto vibovu na  madereva  wanaovunja  sheria  za  usalama  barabarani  inaendelea  kufanyika .

Pia  alisema  kwa  kipindi  hicho  cha  wiki  mbili  jeshi la polisi  limefanikiwa   kukamata  dawa  za  kulevya  pamoja na  watuhumiwa  watano akiwemo Jahati  Kasuga (30) aliyekamatwa na  miche  ya bangi  shambani  kwake kijiji  cha  Ukwega , Davi Mgaya  (37) mkazi wa Changalawe  aliyekamatwa na bangi gram 100, Michi  Balakula (40) mfanyabiashara  na  mkazi wa Zizi la  Ng'ombe aliyekutwa na kete 13  zenye uzito  wa gram 6.5

Watuhumiwa   wengine  waliokamatwa  ni  pamoja na Yahsin Mdem  (33)  mkazi wa  Nyamhanga   akiwa na msokoto  mmoja  wa  dawa  za  kulevya  idhaniayo kuwa ni Heroine  ,Jackson Kalolo (21) mkazi wa  Nyabula  alikamatwa na   shamba la  bangi   lenye  miche 276 yenye  uzito  wa kilogram 6 iliyopandwa  katika shamba la mahindi .

Aidha  jeshi la  polisi  limefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa  wawili  Peter  Nyambigi (40) mkazi  wa Idodi  akiwa na  silaha  aina ya  Gobole kinyume na  utaratibu .

Kamanda  huyo  alisema  kupitia  oparesheni  hiyo  wamefanikiwa  kukamata  wahamiaji haramu 83  Raia wa Ephiopia  ambao  walikuwa  wamejificha katika korongo  kandokando ya  barabara   kuu ya  Iringa  Morogoro  baada ya kushushwa kwenye lori  lenye namba  za  usajili  T903 aina ya  Scania  wakiwa na  wakala  wao  aliyetambuliwa  kwa  jina la  Feruz Nyarusyanjo (18) mkazi  wa  Tukuyu mkoani Mbeya


Aidha  aliwataja  watuhumiwa  wengine  ambao  wamekamatwa  katika  oparesheni  hiyo  wakiwa na  Nyara  za  serikali  kuwa ni  pamoja na  Issack Bernad (37)  mkazi wa Mafinga aliyekutwa na nyama  ya  Swala   wawili  aliowaua kwenye  hifadhi ya Ruaha , , Mohamed  Kayoka (34). mkazi  wa kitisi aliyekamatwa na Nyama  ya Tandala aliyokuwa ameihifadhi  kwenye  ndoo , Antony Mgeni (42)  mkazi wa Makadupa akiwa na kipande  cha mfupa wa Ngiri na magamba mawili ya  kobe bila  kibali.

Kupitia  oparesheni  hiyo Saimon Chaula  aliyekamatwa na  askari  polisi na maofisa  wa TRA  akiwa na  risiti  ya  kughushi  ya  EFDs   yenye namba  100-719-220 iliyokuwa  ikihusishwa na uuzaji wa mbao  zenye thamani ya  shilingi  milioni 5.

Makanya  alisema Charles Kiwale (37) mkazi wa Nduli  alikamatwa na  pikipiki yenye namba za  usajili T730 BSU  aina ya  Sunlg  yenye  chesesi  namba LBRSPJB52B9002572  na  injini namba 11910297 idhaniwayo  kuwa ni  mali ya  wizi  pia  jumla ya watuhumiwa 11 wamekamatwa  kwa kosa la  kunywa  pombe  kabla ya  muda .
TAZAMA CHANEL YA MATUKIODAIMA HAPA  CHINI 0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE