March 27, 2018

RIPOTI YA CAG YAWAFUTA KAZI WAKURUGENZI WAWILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mezani kwake mara baada ya kuzipokea kutoka kwa CAG Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja  zilizowasilishwa katika taarifa hiyo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati viongozi wa Kamati mbalimbali za  Bunge walipokuwa wakizungumza mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa hiyo ya CAG
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya kwenda kuifanyia kazi pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea Ripoti yake Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
15
Baadhi ya Mawaziri waliohudhuri katika tukio la uwasilishwaji wa Taarifa ya Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG wakifatilia kwa makini taarifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
18
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea Taarifa ya Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.
19
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad pamoja na wafayakazi mbalimbali kutoka katika Ofisi yake mara baada ya kuwasilisha taarifa hiyo ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2017, Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
 
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Tarehe 27 Machi, 2018 Amepokea Ripoti Za Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali (CAG) Kwa Mwaka Wa Fedha Wa 2016/17
Tukio La Kukabidhiwa Kwa Ripoti Hiyo Limefanyika Ikulu Jijini Dar Es Salaam Na Kuhudhuriwa Na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu Wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri, Wenyeviti Wa Kamati Nne Za Bunge, Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania (BOT) Prof. Florens Luoga Na Viongozi Wakuu Wa Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama.
Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali Prof. Mussa Juma Assad Amewasilisha Kwa Mhe. Rais Magufuli Ripoti 6 Ambazo Ni Ripoti Ya Serikali Kuu, Ripoti Ya Mamlaka Za Serikali Za Mitaa, Ripoti Ya Mashirika Ya Umma, Ripoti Ya Miradi Ya Maendeleo, Ripoti Ya Ukaguzi Na Ufanisi Na Ripoti 10 Zinazohusu Ukaguzi Wa Ufanisi Katika Sekta Mbalimbali.
Akitoa Mchanganuo Wa Hati Za Ukaguzi Wa Hesabu Katika Serikali Kuu Na Taasisi Zake, Mamlaka Za Serikali Za Mitaa Na Mashirika Ya Umma Kwa Mwaka 2016/17 Prof. Assad Amesema Ofisi Yake Imetoa Jumla Ya Hati 561 Ambapo Kati Yake Hati 502 Sawa Na Asilimia 90 Zinaridhisha, Hati 45 Sawa Na Asilimia 8 Zina Mashaka, Hati 7 Sawa Na Asilimia 1 Haziridhishi Na Hati 7 Sawa Na Asilimia 1 Ni Mbaya.
Prof. Assad Amesema Kwa Ujumla Serikali Imeendelea Kufanya Vizuri Kwani Kumekuwa Hatua Nzuri Zaidi Ya Kuongeza Hati Zinazoridhisha Na Kupunguza Hati Za Mashaka Na Mbaya.  
Amebainisha Kuwa Mashirika Ya Umma Yamepata Hati Safi Kwa Asilimia 96, Mamlaka Ya Serikali Za Mitaa Asilimia 90 Na Serikali Kuu Ambayo Imepata Asilimia 86 Kutokana Na Ndani Yake Kuwemo Vyama Vya Siasa 7 Ambavyo Hakukua Na Makubaliano Juu Hesabu Zake.
Kufuatia Ripoti Hiyo Mhe. Rais Magufuli Amemuagiza Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais, Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo Kuwasimamisha Kazi Wakurugenzi Wa Halmashauri 3 Za Kigoma-Ujiji, Kigoma Vijijini Na Pangani Kutokana Na Halmashauri Zao Kupata Hati Chafu Na Ameahidi Kuwa Serikali Itafanyia Kazi Ripoti Hizo Na Kuchukua Hatua Stahiki.
Kuhusu Kesi Za Rufaa Ya Kodi Zenye Thamani Ya Shilingi Trilioni 4.4 Ambazo Mpaka Sasa Hazijafanyiwa Uamuzi Na Mahakama, Mhe. Rais Magufuli Amemuagiza Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Philip Mpango Kujadiliana Na Jaji Mkuu Ili Kesi Hizo Ziamliwe Haraka.
Baada Ya Kupokea Ripoti Hizo Mhe. Rais Magufuli Amemkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Na Kumuagiza Aitishe Kikao Cha Mawaziri Wote Ili Wazijadili Na Kutafuta Majawabu Ya Hoja Zilizomo.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli Amempongeza Prof. Mussa Juma Assad Na Ofisi Yake Kwa Kazi Nzuri Ya Ukaguzi Wa Hesabu Za Serikali Na Amemhakikishia Kuwa Ushauri Na Mapendekezo Yote Yaliyotolewa Katika Ripoti Hiyo Yatafanyiwa Kazi.
Katika Salamu Zao Wenyeviti Wa Kamati Za Kudumu Za Bunge Za Hesabu Za Serikali (PAC), Hesabu Za Serikali Za Mitaa (LAAC), Uwekezaji Wa Mitaji Ya Umma (PIC) Na Bajeti Wamempongeza Mhe. Rais Magufuli Kwa Juhudi Mbalimbali Anazozifanya Kuwaletea Watanzania Maendeleo Na Wamemhakikishia Kuwa Wataendelea Kuunga Mkono Juhudi Hizo Kwa Kushauri Na Kuisimamia Serikali.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Amewahakikishia Wenyeviti Hao Wa Bunge Kuwa Serikali Itafanyia Kazi Ushauri Walioutoa Ikiwemo Kuteua Na Kuthibitisha Uteuzi Wa Viongozi Mbalimbali Wa Bodi Na Taasisi, Na Kuchukua Hatua Dhidi Ya Watendaji Wenye Dosari.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE