March 31, 2018

RC IRINGA AWAPONGEZA WADAU WAKIWEMO IVORI KWA KUWAKUMBUKA YATIMA PASAKA

Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia  akikabidhi msaada wa Ivori Cocoa Powder kwa  mlezi wa  kituo  cha Yatima  Tosamaganga  leo kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka
Baadhi ya  vitu  mbali mbali  vilivyotolewa kwa yatima  leo
Watu wenye  ulemavu  wakifika  kituoni hapo  kutoa msaada kwa yatima
Mtaalam wa  alama  ishara  akiwaelekeza  watu  wasiosikia wakati wa hafla  ya kutoa msaada kwa yatima  Tosamaganga  leo
Baadhi ya  yatima  kituoni hapo
Baadhi ya  wadau  waliojitokeza  kusaidia yatima  leo

Baadhi ya  bidhaa  zilizotolewa kwa yatima na  walezi  wao  leo  kutoka Ivori
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akiwa na mtoto  yatima
Mbunge  Ritta kabati  akimbusu mtoto  yatima  kwa  upendo
Misaada ya pesa kutoka kwa  wadau mbali mbali  wakimkabidhi mkuu wa  mkoa wa Iringa
Mwakilishi wa  mkurugenzi Manispaa ya  Iringa Dkt Nyenza  akitoa msaada
Kamanda wa  polisi mkoa wa Iringa  Juma Bwire  akitoa msaada  wake kwa ajili ya yatima
Mwakilishi wa Iruwasa  akitoa  msaada
mmoja  wa wakurugenzi wa shule  binafsi  wilaya ya  Kilolo Bw  Francis Mwilafi akitoa msaada  wake
Misaada kwa yatima Tosamaganga
Baadhi ya  misaada
Mtoto  yatima  akikabidhiwa  mbuzi ya pasaka la mkuu wa mkoa wa Iringa
Mkuu wa  mkoa wa Iringa wa  tatu  kushoto ,mbunge Kabati na katibu wa UWT mkoa wa Iringa wakikabidhi mbuzi
mkuu wa mkoa akikabidhi mbuzi iliyotolewa  zawadi kwa yatima
Mkuu wa  mkoa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama
Mbunge Kabati  akitoa  neno
SERIKALI ya  mkoa  wa  Iringa imepongeza  wadau  mbali mbali  kikiwemo  kiwanda cha kiwanda cha Ivori Food & Bevaragena  chini ya mkurugenzi Mtendaji Suhail Esmail Thakore kwa  kuitikiwa  wito  wa ofisi yake katika  kuwasaidia watoto  yatima  wa kituo cha Tosamaganga misaada ya Pasaka .
Hatua  hiyo  imekuja  baada ya  kuwepo kwa  mwitikio mkubwa wa  wafanyabiashara  na makampuni mbali mbali likiwemo la  Ivori , Ruaha Milling Compuny Ltd  pamoja na taasisi kama  Iruwasa , shule ya  wasichana Iringa na  wengine  kuunga mkono uchangiaji wa yatima  hao leo.

Akizungumza  leo wakati wa  kukabidhi  misaada  hiyo  kikiwemo  chakula ,nguo , sabuni pipi za Ivori ,Cocoa Powder  na vingine kama mbuzi na unga na mchele ,mkuu   huyo wa  mkoa  alisema  amefarijika  sana  kwa  kuitikia wito  huo mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema amefarijika  sana kwa misaada  hiyo.

Kwani  alisema  mwitikio huo ni mkubwa na unawafanya  watoto  hao yatima kutojisikia  wanyonge wakati wa  sikukuu  na kuwa  watoto  hao watasherekea Pasaka vizuri .

Aidha  mkuu  wa  mkoa amewataka wadau  mbali mbali na  wananchi wa  mkoa wa Iringa  kuendelea  kujenga  utamaduni wa  kuwajali  watoto yatima  wakati wa  sikukuu mbali mbali  ili nao  waweze  kujumuika na  wenzao  wenye wazazi  kufurahia  sikukuu  hizo.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE