March 27, 2018

RC IRINGA ACHUKIZWA NA MFANYABIASHARA HUYU KUFUNGA TRANSFOMA ENEO HATARI AAGIZA LIONDOLEWE

Hii  ndio  Transifoma  inayolalamikiwa  ambayo  imefungwa  eneo la kona barabarani na  eneo la maegesho ya gari ya  kiwanja  namba 6 
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza amekasilishwa na uwekaji  wa  Transfoma  kibabe  katika  eneo  la uchochoro  lenye  kona kali eneo la  Stendi  kuu ya Manispaa ya  Iringa ambako  limejengwa  jengo la  Ghorofa  linalomilikiwa na  Aisen Msigwa .
 Mkuu  wa  mkoa na  viongozi  wa  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa pamoja na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  walifika  eneo  hilo  baada ya  kuwepo malalamiko  mengi  kutoka kwa wananchi wakilalamikia Transfoma  hiyo  kuwa  eneo hatarishi .

 Akizungumza  eneo la  tukio mkuu  huyo wa  mkoa  aliagiza  uongozi wa Tanesco  Iringa  kutazama  uhalali  wa  Transfoma   hiyo  kufungwa  eneo   hilo  lenye  kona   na kama  si  halalli  basi  kuliondoa katika  eneo  hilo huku  akitaka  ofisi ya  mipango  miji  kushughulikia  kutatua  kero  hiyo ya  wananchi  kwani  kuacha   Transfoma  hilo  eneo  hilo ni hatari  zaidi kwa  usalama wa  wananchi wanaozunguka  stendi hiyo.

Pamoja  na  mkuu  huyo wa  mkoa  wa Iringa  kuagiza  Transfoma   hiyo  kutolewa  eneo  hilo hatari  mtandao  wa matukiodaima  umeshuhudia upuuziaji wa  agizo la mkuu wa  mkoa  kwani toka  alipotoa  agizo  hilo  jumapili  hakuna hatua  zinazochukuliwa huku  wananchi  wakitaka  agizo la  mkuu wa  mkoa litekelezwe haraka  .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE