March 8, 2018

MWANAFUNZI ALIYETEKWA DAR APATIKANA MAFINGA JANA USIKU

Viongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi kilichoko karibu.
Mahojiano yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe, baba mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kutekwa kwake.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE