March 9, 2018

MBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA ASHINDWA KWA HOJA NA MBUNGE KABATI HOJA KUTETEA WANANCHI KUPIGWA FAINI

Mbunge  Mchungaji  Peter  Msigwa (chadema)  kulia  akijiandaa  kumpongeza  mbunge  wa  viti  maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kushoto  siku  alipoapishwa bungeni mjini Dodoma
Mbunge wa  jimbo la  Iringa  mjini Mchungaji Peter  Msigwa (Chadema) kulia na mbunge wa Kilolo Venance  Mqwamoto (CCM)  wakimpongeza  mbunge wa  viti maalum mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) siku alipoapishwa kuwa  mbunge  (picha na maktaba ya  matukiodaima)
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE  wa   viti maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta kabati  (CCM) na  mbunge  wa  jimbo la  Iringa  mjini  mchungaji  Peter  Msigwa  wavutaka  katika  kikao  cha bodi ya  barabara  mkoa  wa  Iringa  baada ya  mbunge Kabati  kumtaka kaimu  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  kueleza  tarehe  kamili ya  stendi mpya  kuanza  kutumika .
Katika  kikao  hicho  kilichofanyika  ukumbi wa  siasa ni  kilimo  juzi na kuongozwa na mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  mbunge Kabati  alihoji ni  lini stendi   mpya ya  Igumbilo itaanza  kutumika  baada ya  kuwepo  ili  kuwaepusha  wenye magari  wanaoegesha magari yao kando kando ya  barabara  kuu  ya  Iringa – Dodoma   kupigwa  faini ya  200,000 na  wakala  wa barabara  (TANROADS ) kwa  kuegesha magari  yao  maeneo yasiyoruhusiwa .
Baada ya  swali  la mbunge  huyo kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Omary Mkangama  alieleza  kikao  kuwa  stendi hiyo imekamilika awamu ya kwanza na  itaanza  kutumika wakati wowote japo   changamoto ni  upatikanaji wa  fedha  za  kuchonga  barabara  ya  kufika  stendi hapo  .
Kutokana na majibu hayo  mwenyekiti wa  kikao  hicho  mkuu wa  mkoa wa Iringa kama  alimhoji  mbunge Kabati kama  ameridhishwa na  jibu ,mbunge  huyo huyo alitaka  kujua  ni tarehe  ngapi  stendi itakamilika .
Kufuatia  swali  hilo  mbunge  mchungaji  Msigwa  alisimama na baada ya  kupewa nafasi ya  kuulizwa  swali  na  mwenyekiti wa  kikao  hicho ,mbunge Mchungaji Msigwa alimtaka  mbunge  Kabati swali   hilo alipelekea  kwenye  kikao  cha baraza la madiwani  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa sio kwenye  kikao   hicho .
Kauli  hiyo ya  mchungaji  Msigwa  ilimfanya mbunge Kabati  kusimama na  kumjibu mbunge  Msigwa  kuwa  swali  hilo limeulizwa kwenye  kikao  hicho  kwani ndicho  kikao  chenye uamuzi wa  kuendelea  kuwapiga  faini  wananchi wanaoegesha magari yao  kando kando ya barabara  na  kujulikana  tarehe ya  kumalizika kwa  stendi  hiyo  ni  suluhisho  la wananchi  kuendelea  kutozwa  faini .
Mvutano  wa  wabunge hao  ulipelekea  mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  kuingilia kati na  kueleza kuwa  stendi  hiyo ya Igumbilo haitakamilika  mwezi  huu labda mwezi wa tano  kwani katika bajeti  yake ya  awamu ya kwanza ya pili nay a tatu  hakuna pesa ya  utengenezaji wa barabara .
Katibu  wa   chama  cha mapinduzi  (CCM)  mkoa wa  Iringa Christopher Mgalla  alishauri  uwepo utaratibu wa  kuwaachia kwa  muda  wenye  magari  kushuka kuegesha magari yao katika barabara  ya Iringa – Dodoma  japo kwa  dakika  20  ili  kupata mahitaji katika maduka  yaliyopo kandokando ya  barabara   hiyo  ushauri  uliopokelewa na mwenyekiti wa kikao   hicho Amina Masenza na  wajumbe wote .
 Huku  mbunge  Mchungaji Msigwa akiunga mkono  hoja ya  katibu  huyo wa CCM kwani alisema  itasaidia  kupunguza  kero  kwa  wananchi .
“ Napenda  kuungana  na katibu wa CCM kwa  ushauri  huu  nami  napendekeza jambo  hilo  lifanyike  ili kuondoka kero kwa  wananchi  wetu “
Katika  hatua  nyingine  wajumbe wa  kikao  hicho   wataka  wakala  wa  barabara  vijijini ( TARURA)  na  Tanroads  kuangalia  uwezekano  wa  kutekeleza   ujenzi wa  barabara  za lami katika maeneo  korofi pamoja na  kutekeleza ahadi  iliyotolewa na Rais  wa awamu ya nne na wa  tano  iliyopo katika Ilani ya  CCM ya  ujenzi  wa barabara  ya  kiwango  cha lami kutoka  Ipogolo kwenda  Kilolo na ile ya Mafinga – Kibao  wilayani Mufindi .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE