March 12, 2018

MBUNGE MSIGWA AMVAA LUSINDE...MBUNGE  wa  jimbo la  Iringa  mjini mchungaji Peter  Msigwa ( Chadema) amshangaa mbunge  wa Mtera Livingstone Lusinde (Kibajaji)  kujisifia  kuwa na  namba ya  simu ya  Rais Dkt  John Magufuli  wakati  jimboni kwake  hakuna maji   safi na  salama .

Akiwahutubia  wananchi  wa jimbo  la  Iringa  mjini katika  mkutano  wake uliofanyika  juzi  uwanja  wa  Mwembetogwa  ,mbunge  mchungaji  Msigwa  alisema  anawashangaa  baadhi ya  wabunge  wa chama  cha mapinduzi ( CCM)  ambao  wamekuwa  wakijisifia   kuwa na namba  ya  simu ya Rais Dkt  Magufuli  namba  ambayo  haiwasaidii  kutatua  kero  kwa  wananchi  wao .

" Ujue  hawa  wabunge  wa  CCM mimi  nawashangaa  sana  mfano  nilikuwa katika kampeni  za  ubunge  jimbo la  Kinondoni aliyekuwa  mgombea  wa  CCM  akisimama jukwaani na  mwenzake  Kibajaji  wanawaambia  wananchi  sisi tuna namba  ya simu ya  Rais hivyo tuamini sisi  sio  hao  wapinzani sasa  kuwa na  namba  ya  simu ya Rais ni maendeleo mbona Kibajaji ana namba ya  simu ya  Rais jimboni  kwake  wananchi hawana maji ila  mimi hapa  Iringa mjini  sina namba ya  simu ya Rais  ina wananchi  wangu  wana maji  safi na  salama"

Alisema  kujisifia  kuwa na  namba ya  simu ya  Rais  wakati  wananchi  wao majimboni hawana  maji ni  ufinyu  wa  fikra  na  kuwataka  wananchi  kuzidi  kumwamini yeye  kwani hana namba ya  simu ya Rais  ila amekuwa akifanya  makubwa   jimboni .

Mbunge   huyo alisema  kuwa amepata  kumsikia  Rais  akiwa  ikulu  akizungumzia  akizungumzia  suala la machinga  kutonyanyaswa hoja  ambayo  yeye  aliianzishwa mwaka 2013 alisema  bungeni kuwa  machinga  watengewe  mitaa kwa  ajili ya kufanya  shughuli  zake.

"  Nilipotoka bungeni  nikiendelea  kuwatetea  machinga  hawa  huku jimboni nilipigwa mabomu na hata  kukamatwa  kuwekwa  ndani ila  leo hawa machinga   ni  wanafiki  wakubwa  wanasimama  kusifia  CCM  wakati  mimi  niliwekwa ndani na kupigwa mabomu  nikiwatetea  wao" 

Mbunge  Msigwa  alisema  ili  wananchi katika chaguzi nyingine  waweze  kuchagua  watu  ambao  wanawasaidia  ni  vizuri katiba ya  jaji  Warioba ikaharakishwa  ili wagombea  wasio  na  sera  kama akina  Kibajaji na  wenzake   kutochaguliwa .

Alisema  kuwa ubunge  wake  hajawekwa na  mtu  bali  amepewa na  Mungu  aliyejuu hivyo  akiamua  kumtoa atamtoa na  asipo amua  Mungu  hakuna  mtu  wa  kumtoa  ubunge  wake  kwani mipango ya  binadamu  haiwezi  kumzidi  Mungu  aliyejuu .

Hata   hivyo  alisema  kuwa  CCM  Iringa  wamekuwa  wakitafuta  kiki  kupitia  yeye  kwani hivi  sasa  wametoa  TV moja katika  soko  kuu la  Iringa mjini  wakidai  wanatimiza ahadi yake aliyoitoa  ya kufunga  TV  sokoni hapo  na  kuwa TV iliyotolewa na  CCM ni ahadi yao wenyewe  kwani  yeye  aliahidi  kufunga  TV 10  katika  soko  hilo na atatekeleza ahadi  hiyo  ndani ya mwaka  huu kabla ya  kuanza fainali ya  kombe la Dunia .

"  Hawa  jamaa  wa  CCM uwezo wao  wa  kufikiri ni mdogo  sana  kuna  wakati  mimi  niliahidi  saruji  mifuko 100  Nduli  katika  ubunge wangu uliopita wakaona Msigwa atapata  sifa   wao  wakaenda  kukabidhi  mifuko 200 leo wameenda  kukabidhi  TV  moja  wakati  mimi  niliahidi TV 10  kweli  hawa  jamaa uwezo wao wa  kufikiri ni mdogo  sana na  wanafikiri  wanaweza  kunitoa mimi  ubunge hapa  Iringa mjini  wanapoteza  muda wao  bure  hawaniwezi "

"  Hivi  vyeo  ni  dhamana  tu  nimemwambia  kamanda  wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Juma  Bwire  atende  haki haiwezekani kuniletea askari  wote  hawa kuja  kwenye  mkutano  wangu  kutisha  wananchi  ulinzi ambao ni  mkubwa kuliko hata ule wa mkutano wa makamu wa Rais alioufanya katika  uwanja  huu "

Katika  mkutano huo  wananchi  walimwomba  mbunge  Msigwa akienda  bungeni  ahoji  juu ya  ahadi ya  Rais Dkt  Magufuli ya  milioni  50  kila  kijiji  zitatolewa  wakati gani pamoja na kutaka  serikali  kutoa  tamko la kukemea  watu  kutekwa na  watu wasiojulikana .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE