March 14, 2018

MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSIMI UJENZI WA RELI YA KISASA DODOMA

ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli kesho tarehe 14 Machi, 2018 ataweka jiwe la msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.
Sherehe za uwekaji jiwe la msingi zitafanyika kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Ihumwa nje kidogo ya Mji wa Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wananchi wa Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli hapa nchini Bw. Masanja Kadogosa anasema maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi katika sherehe hizo yamekamilika na amewataka wananchi kujitokeza katika sherehe na waliombali na Dodoma kufuatilia matangazo yatakayorushwa hewani na vituo vya redio na televisheni
Hii ni sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya awamu tano zilizopangwa kukamilisha ujenzi wa reli hiyo itakayoanzia Dar es Salaam hadi Mwanza.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE