March 29, 2018

LOWASSA AONGOZA WANACHAMA KISUTU

Mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye amehudhuria katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kufuatilia hatma ya kesi ya viongozi 6 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe kama watapata dhamana au wataendelea kusota rumande.
Viongozi sita wa Chadema wamefikishwa leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao, huku ulinzi ukiimarishwa katika eneo hilo.

Kesi hiyo inatajwa leo Machi 29, ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard, Mashauri atatoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana au hawatapata.

Wakati viongozi hao wakifikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi kuzunguka viunga vya mahakama ya Kisutu.

Katika lango kuu la kuingia mahakamani hapo, polisi waliovalia kiraia walifanya ukaguzi kwa kila anayeingia na kutoka na kuwazuia baadhi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE