March 30, 2018

KKKT DAYOSISI YA IRINGA ,YAELEZEA WARAKA WAKE

Msaidizi  wa askofu kanisa la  kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya  Iringa Himid Saga akihitimisha  ibada ya ijumaa kuu leo asubuhi
Waimbaji wa kwaya ya Muhimidini wakiimba  wimbo maalumu wa ijumaa kuu
Baadhi ya  wageni  waliofika kanisani hapo
Wageni  hao  wakionyesha zawadi ya mishumaa
Mkuu wa jimbo akionyesha  mishumaa iliyotolewa kama  zawadi na wageni hao kutoka  Sweden
Waumini  wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu wakiwa katika ibada ya Ijumaa kuu leo
Idaba  ya ijumaa kuu


WAKATI  jamii ikiwa inahamu ya  kujua  juu ya  waraka  unaokusudiwa kusomwa na makanisa  mbali mbali  ya  Kikristo  likiwemo kanisa la  kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT)  

Msaidizi  wa askofu wa  KKKT Dayosisi ya  Iringa  Himidi Saga  amesema   kuwa waraka  ambao unakusudiwa  kusomwa wakati wa kumbukumbu ya  Pasaka  kwa  waumini  wa  kanisa  hilo ni  waraka  wa  kitume na utasomwa katika makanisa yote .

Saga  aliyasema  haya  leo  nje ya  kanisa kuu la usharika  wa Iringa mjini mara  baada ya  kumalizika  kwa  ibada ya  ijumaa  kuu wakati wa mahojiano na mtandao wa matukiodaimaBlog ,alisema   kuwa  ni  kweli  upo  waraka ambao umetolewa na kanisa  hilo kwa makanisa  yote kwa  ajili ya  kusomwa mbele ya  waumini  wake .

“ Kwanza  nishukuru  kwa  ajili ya  nafasi  ambayo  tumepewa  kwa  ajili ya  kumbukumbu ya  kifo cha bwana  wetu  Yesu Kristo  niombe  sana wakristo  wote na  wasio  wakristo  kuiona  siku  hii ni njema sana katika  kuponya  nafsi zao   kwa  kuwa  kupitia  sikukuu  hii ndipo  tunapata nafasi ya kuweka huzuni  zetu  mbele za Mungu  kanisa  letu Pasaka  hii litakuwa na tamko ambalo limesambazwa maeneo mbali mbali “

Alisema   kimsingi  waraka huo wa maaskofu  utasomwa  siku ya  jumapili na  kuwa siku  hiyo  ndipo  kitajulikana  nini  kimesemwa na  maaskofu  kwenye waraka  huo kwani kwa sasa haujafunguliwa .

Hivyo  alisema kupitia ibada  hiyo ya  ijumaa kuu  anawaomba  waumini  kujiandaa  kwa  kusikia kilichoelezwa  kwenye waraka huo  kwani  waraka huo umekwisha  fika  na  maelekezo yaliyotolewa unapaswa  kusomwa siku ya Pasaka  yenyewe  ambayo ni  kumbukumbu ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

“ Pamoja  na  kuwa waraka huu  una kurasa kama nane   hivi   wakati   fulani ni  ngumu  kusoma  kurasa  zote  lakini  hatujaweka  utaratibu  njia  zipi  tutatumia  kuusoma  lakini  lazima usomwe  kama  tulivyoelekezwa  maana  ibada  zetu zinatakiwa  kwenda kwa ufupi hivyo kama tutasoma ama  kubandika ama vinginevyo  waumini watajulishwa”

Habari  zaidi  soma gazeti la Mtanzania Kesho  jumamosi ama tembelea chanel ya Youtube ; matukiodaima 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE