March 30, 2018

JESHI LA POLISI IRINGA LATUMA SALAMU ZA PASAKA KWA WATAKAO VURUGA SIKUKUU KUKIAONA


                                                             RPC -JUMA BWIRE
................................................................................................................................................
              Na MatukiodaimaBlog
JESHI  la Polisi mkoa wa Iringa limetuma  salamu za Pasaka kwa wananchi  wote  kwa  kuwataka  kusherekea sikukuu ya Pasaka katika hali ya amani na utulivu na kuwa jeshi hilo halitamvumilia mtu ama kikundi chochote kitakacho vuruga amani wakati wa Pasaka .

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wamiliki na watoa huduma wa vyombo vya usafiri kwenye ukumbi wa siasa ni Kilimo wakati wa warsha ya kujikumbusha sheria za SUMATRA .

 Alisema kuwa nyumba zote za ibada kwa siku ya jumapili wakati wa sikukuu za Pasaka zitawekewa ulinzi mkali ili kuepusha waharifu kufanya uharifu ,pia jeshi hilo litawachukulia hatua kali wale wote watakaofanya biashara ya Disco toto kwani hakuna ruksa ya kufanya hivyo.

 Kuhusu madereva kamanda huyo aliwataka kujiepusha na ulevi
wakiwa katika vyombo vya moto na kuwa dereva ambaye atakutwa akipiga honi ovyo atakamatwa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE