March 5, 2018

ISLAMIC STATES YASAMBAZA VIDEO ZA MAUAJI KWENYE MITANDAO

Video zilizosmbazwa na IS


Wapiganaji wa kundi la Islamic State IS wamesambaza picha za video zinazodaiwa kuonyesha mauaji ya wanajeshi wane wa Marekani waliouawa nchini Niger mwezi Octoba mwaka mwakajana.
Hata hivyo haijajulikana mara moja kwanini picha hizo zimetolewa kwa kuchelewa hadi,ambapo zimetolewa kupitia program ya kimtandao ya Telegram
Picha hizo zilipigwa na mmoja wa wanajeshi wa Marekani kupitia kamera yake ya siri aliyokuwa nayo kwenye kofia yake ngumu aliyokuwa ameivaa yaani Helmet.
Lengo la video hizo ni kutaka kubainisha kwamba IS ndiyo waliofanya shambulio hilo.
Picha zinazo onekana zinaanza na zile za mnato ambazo baadhi ya wapiganaji hao wakitoa kiapo cha utii kwa kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi mtandao huo wenye makundi yenye utiifu kwa IS kama vile Sahel,Jamaat Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM).
Kwa mjibu wa BBC video hizo zinawaonyesha wapiganaji hao wakitembea na kukimbia jangwani kuelekea kufanya shambulizi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE