March 31, 2018

CHONDE CHONDE MAASKOFU MSISOME KESHO WARAKA WENU PIGINE MAGOTI TUOMBEENI - MBUNGE RITTA KABATI

 
 Na  MatukiodaimaBlog
WAKATI  kesho makanisa  mbali  mbali ya kikristo nchini yanatarajia  kutumia ibada ya sikukuu ya Pasaka ambayo ni maalum  kwa  ajili ya  kumbukumbu ya  kufufuka kwa  Yesu Kristo ,kusoma  waraka maalum  kwa Taifa , mbunge  wa  viti  maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM)  amewaomba maaskofu nchini  kusitisha kusoma  waraka  huo na badala  yake  kupiga magoti  kuliombea Taifa.

Kuwa  kila  mmoja anapokea  tofauti matamko  hayo  hivyo  wanaweza  kusema  wanafanya  kwa utume wa  Mungu  kumbe  wakavuruga  utume  wa Mungu kupitia matamko  hayo makanisani ni  vema  wakapiga magoti ya  kusali sio  kusoma  waraka  huo  wasome Biblia kusherekea  kufufuka kwa Yesu kristo.

Akizungumza leo   na  wanahabari  wakati  zoezi  fupi na ofisi ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza kuwaongoza  wananchi wa  mji wa Iringa kukabidhi  misaada mbali mbali  ikiwemo ya  nguo na chakula kwa watoto  yatima  wa  kituo cha Tosamaganga ,mbunge Kabati  alisema  kuwa waraka  huo wa maaskofu umezua   hofu  kubwa kwa  wananchi na kila mmoja kutaka  kuusikia  japo  aliomba hekima  ya maaskofu  kutumika katika suala  hilo .

" Sio  kwamba nawapangia majukumu ya kufanya  maaskofu  na  viongozi wangu wa  dini ila naomba zoezi hili la  waraka  kusitishwa  kusoma  makanisani na badala yake viongozi hao  wa  dini kufanya kazi ya  kuliombea  Taifa na  watu wake badala ya  kutoa  waraka"

Kabati  alisema  kuwa  jukumu  kubwa la  viongozi wa  dini  ni kueneza  injili na watu  wakakombolewa  kupitia  injili na  sio  kuwafanya  watu  kuwa na  hofu kama  iliyowekwa na viongozi hao wa dini  kupitia waraka   huo ambao haujulikani una nini ndani yake kwa Taifa kwani ni  waraka ambao  umekuja ghafla  umeanza  kuzua mgawanyiko  hata  miongoni mwa dhehebu  moja  hadi jingine na askofu  mmoja  na mwingine jambo ambalo  si  sahihi .
Mbunge  huyo  alisema  ingependeza kwa  maaskofu hao na  viongozi  wengine wa  dini za  kikristo  kwa  wakati  huo  wa  Pasaka ambao ni  wakati kusherekea  kufukuka kwa  Yesu  Kristo na  wakati wa ule  wa  mateso ya  Yesu  wangejielekeza  zaidi katika  kuzama katika maombi ya kuliombea  Taifa  ili  waumini  wao wafanye kazi za  kusambaza  upendo na  kuwasaidia  watu  wenye mahitaji kama yatima na  wengine  waliokosa faraja  kuliko kuwaandaa kuujua waraka  huo .

" Tayari  baadhi ya makanisa  wamekwisha toa waraka  ambao  pamoja  na kuwa  walidai ni waraka mwema  ili  umeonekana ni  waraka  wa mlengo furani ambao unawagawa hata  waumini  wao ambao wapo  upande  ambao  wao wanauunga  mkono chonde  chonde viongozi wa dini ni  vizuri  kuwaelekeza waumini wenu  kuyajua  maandiko na kuomba kwa ajili ya wenye shida  kuliko kukimbilia  kutoa  waraka  hata  Biblia  imesema ya Kaisali mwachie  Kaisali na ya  Mungu mwachia Mungu sasa badala ya  kutoa matamko  wao  wangetuombea  haya matamko yanapokelewa  tofauti "
Hata  hivyo  mbunge  huyo  alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Mazenza kwa hatua ya  kuwaunganisha  pamoja wadau mbali mbali na  wananchi wa mji wa Iringa kwenda  kusaidia watoto  yatima  Tosamaganga  na  kuwa utamaduni  huo  unapaswa  kuwa  endelevu katika  sikukuu zote za kikristo na kiislamu kwani umeanza  vizuri .

Kwa  upande  wake  mkuu wa  mkoa wa Iringa Masenza  mbali ya  kuwapongeza wananchi  mbali mbali  na  viongozi wa CCM na serikali  na  wafanyabiashara  mkoani hapo  kujitokeza  kuungana kwenda kusaidia  yatima  hao bado  alisema suala la upendo linahitajika  kuwa endelevu na  kuwa   ofisi yake  imelazimika kuratibu  zoezi hilo la kwenda kusaidia yatima  ili kuwafanya nao washerekee Pasaka kama watoto  walio na wazazi wao .

Alisema  pamoja  na  vitu  mbali mbali ambavyo  vimechangwa kwa  ajili ya  watoto hao  pia kuna mbuzi ,mafuta na  kula ,nguo ,sabuni ,pipi toka Ivori  pamoja na pesa kiasi cha  zaidi ya  shilingi 450,000 zilizotolewa na  wadau hao kwa ajili ya watoto hao .

Aidha  mkuu huyo wa  mkoa alitaka  wananchi  wa mkoa wa Iringa kusherekea  sikukuu  hiyo kwa amani na utulivu na kuwa ofisi yake  kupitia  vyombo  vya ulinzi na usalama na  vyombo  vya sheria  hataacha kuchukua hatua kali kwa  mwanaume  yeyote  atakaye lewa  pombe na  kumpiga mke wake wakati wa sikukuu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE