March 24, 2018

CCM IRINGA MJINI WAMTANGULIA MBUNGE MSIGWA WAKABIDHI TV NYINGINE SOKO KUU ,WAFANYABIASHARA WATOA NENO

Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya na mwenyekiti wa soko Julia wakizindua TV 5 walizofunga soko kuu 
Wananchi na wafanyabiashara wakitazama TV
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya akionyesha maeneo ya kufunga TV 
Mwenyekiti wa soko kuu akikabidhiwa TV 5 na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya
Mwenyekiti wa CCM akikabidhi vifaa vya TV 
TV zilizofungwa na CCM soko kuu

WAKATI mbunge wa jimbo la IRINGA mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) akiendelea kutoa ahadi isiyotekelezeka ya TV 10 alizoahidi soko kuu la manispaa ya Iringa ,CCM Iringa mjini wamemtangulia kwa kufunga TV Kila kona ya soko.

Akikabidhi TV tano kubwa  zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 ,mwenyekiti was CCM Iringa mjini Said Rubeya alisema wajibu wa CCM ni kutatua kero za wananchi .

Hivyo alisema wataendelea kusaidia kutatua kero za wananchi na kuwa TV hizo ziliahidiwa na mbunge Msigwa wakati wa kampeni pasipo kutekeleza ahadi hiyo kama alivyoitoa.

"Tumeona ni vema kutatua kero ya wananchi kama ambavyo walivyotuomba kupitia viongozi wao wa soko kuwa hitaji lao ni TV na kwa kuwa mbunge kashindwa kutimiza CCM tumeombwa kutekeleza "

Mwenyekiti Hugo alisema kuwa wao kama CCM hawapendi kudanganya wananchi hivyo wataendelea kufumbua kero zote za wananchi bila kujali zimetolewa na wananchi wa chama kipi.

"Huu ni wakati wa kazi na kuwaletea wananchi maendeleo sio wakati wa siasa na porojo za majukwaani tunachapa kazi "

Hats hivyo alimtaka Mbunge Msigwa kuacha kuwadanganya wananchi na ahadi hewa na kuwa siasa anazozifanya za kutukana na watu na kuwajengea wananchi chuki ni siasa za ovyo.

Kwa upande wao wafanyabiashara sokoni hapa akiwemo Maonyesho Msigwa alisema kuwa ahadi hivyo ya TV ilitolewa na mbunge Msigwa wakati wa kampeni ila imekuwa haitekelezwi zaidi ya maneno kila wakati ni ahadi juu ya ahadi .

"Tumechoka na uongo wa ahadi hewa ya mbunge wetu ,CCM walipofunga TV moja kubwa kuanza kutekeleza ahadi iliyotolewa na mbunge wetu yeye aliitisha mkutano na kujinasibu kuwa atatoa TV 10 Ila hadi leo hata TV moja kashindwa kufunga zaidi ya ahadi tele"

Alimtaka mbunge kuacha kuahidi na kudanganya kuwa soko linavuja wakati soko hilo ni zima kama linavuja mbona wao wanafanyabiashara na hawanyeshewi mvua.

Pia alieleza kusikitishwa na kauli ya mbunge Msigwa kuhusu wananchi kususia bidhaa za wafanyabiashara wanaokiunga mkono chama cha mapinduzi kuwa ni siasa za chuki na hawaziungi mkono.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega alisema kuwa kazi inayofanywa na CCM Iringa mjini imelenga kuwakomboa wananchi na kuwa mbunge Msigwa hajafanya chochote jimboni hapo toka alipochaguliwa .

"Mimi ndio nilikuwa mbunge hapa kabla yake na miradi yote inayoendelea ni ile ambayo niliianza mimi japo nasikitika kuona baadhi ya miradi imesimama kama mradi wa machinjio ya kisasa huyu ni mbunge wa maneno sio maendeleo"

Kwani alisema akiwa mbunge alishaombwa TV sokoni hapo na alitoa moja na Leo anashuhudia CCM wakiendelea kukabidhi TV zaidi .

Kada wa CCM Michael Mlowe ambae alipata kuingia katika kinyang'anyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea ubunge mwaka 2015 ,alimtaka Msigwa kuacha kauli za kichochezi juu ya kutaka wananchi kususia bidhaa za wanaounga mkono serikali na CCM .

Kwani alisema hao wanaounga mkono CCM ndio ambao wamejenga mawodi na kuleta maendeleo kwa wananchi .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE