March 24, 2018

AJALI YAUA MBILI ZAUA WATU SABA IRINGA

Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire akitazama daladala iliyoua saba Iringa

WATU  saba  wamefariki   dunia kwa  ajali  mbali  za  gari  ziliotokea  usiku  wa  kuamkia  leo katika  Manispaa ya  Iringa  mkoani  Iringa .

Mashuhuda  wa  ajali  hiyo iliyotokea katika  eneo la Igumbilo  mjini  Iringa kwenye  barabara  kuu ya Iringa – Morogoro walimweleza  mwandishi  wa  habari  hizi  kuwa chanzo  cha  ajali  hiyo  ni  uzembe  wa  dereva  wa  daladala  ambaye  aliendesha   gari lake  kwa  uzembe  na  kuingia  nyuma ya  lori  lililokuwa  limeharibika .

John Sanga  ambae  ni  mmoja kati ya abiria  walionusurika  katika  ajali  hiyo  alisema  kuwa  dereva  wa daladala   hiyo  alikuwa  akifukuzana na  daladala  nyingine  akitaka  kuwahi  kupakia  abiria  kituo  cha  Igumbilo .

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  akizungumza  eneo  la  tukio  mbali ya  kuwapa  pole  majeruhi  na waombolezaji  waliopoteza  ndugu  zao aliliagiza  jeshi la  polisi  kumsaka dereva  wa daladala   hiyo  pamoja  na  kuchunguza bima   ya  daladala  hiyo  ili  majeruhi  na waliopeteza  maisha  waweze  kufidiwa .

Akithibitisha  kutokea  kwa  ajali  hiyo  kamanda  wa   polisi  wa  mkoa  wa  Iinga  Juma Bwire  alisema  ajali  hiyo ilitokea  majira  ya  saa  1;30 jana  ilihusisha  daladala yenye  namba  za  usajili T 891 Toyota  Hiace mali  ya Antilio Makagula ikiendeshwa  na  dereva  ambaye  bado hajafahamika    ikitokea  mjini Iringa  kwenda  Viwengi  wilaya ya  Kilolo  liliingia  nyuma ya  lori lenye  namba T974 AKF Scania  mali ya Nelly Investment ya  Dar es Salaam  lililokuwa  limeharibika na  kusababisha  vifo  vya  watu watano  papo  hapo  na  mmoja  na  kujeruhi watano kufia  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa akipatiwa matibabu .

 Katika  ajali ya   pili  iliyotokea  eneo la Wenda  wilaya ya  Iringa  kwa  gari  yenye namba za  usajili  DFPA 3256  aina  ya Ford Ranger  mali  ya Fintrac Tanzania ikitokea  Mafinga  kuelekea  mjini  Iringa lilimgonga  mtembea  kwa  miguu Sabra Abdul  (4)  mwanafunzi  wa  darasa awali Wenda   kuwa  mwanafunzi huyo alifia  njiani akikimbizwa  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa 


 kuwa  dereva  wa  gari hilo Zephania Wiliam (28) amekamatwa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE