March 24, 2018

AJALI YAUA IRINGA ,MWENYEKITI WA KAMATI YA USALAMA BARABARANI ,AONYA MADEREVA KUWA MAKINI

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas kulia  akimpa pole Diwani wa Nduli Bashir Mtove kwa msiba wa mtoto wake aliyepata ajali ya gari lililoua watu zaidi ya sita jana

Asas akimpa pole Diwani Mtove anayefuata nyuma ni katibu wa Itikadi NA uenezi Mkoa wa Iringa Ramadhan Baraza


Viongozi wa Ccm wakiwa NA Mnec Salim Abri kulia alitekuwa Diwani Kwakilosa Kupitia Chadema Joseph Lyata,Diwani Mtove na Baraza 
Asas akiwapa pole majeruhi hospitali ya Mkoa Leo
MWENYEKITI wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas Leo amewatembelea kuwapa pole wafiwa wa ajali iliyoua sita Iringa na mejeruhi.

Pamoja na kuwapa pole wafiwa Asas amewaonya madereva kuwa makini na kuepuka kuendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa ama kuvuta bangi.

Alisema ajali hiyo ni ajali kubwa ya kwanza kwa mwaka huu na chanzo ni uzembe wa dereva na ulevi .

Hivyo amelitaka jeshi la polisi kuendelea kuwabaini madereva walevi na kuwachukulia hatua.

Kwani alisema vifo vya watu hao vimeacha simanzi kubwa katika Mkoa wa Iringa na kuwa Iringa bila ajali inawezekana.

Kwa upande wake katibu wa itikadi na uenezi CCM Mkoa wa Iringa Ramadhan Baraza aliyeongozana na mwenyekiti huyo kutoa pole pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wametaka jeshi la polisi kumsaka dereva huyo .

Baraza alisema wamepokea kwa simanzi kubwa vifo hivyo na kuwa wanaungana na wote wenye majonzi na kuwaombea majeruhi kupona .

Huku Mkuu wa Mkoa wa Iringa akitaka polisi kuendelea na msako wa madereva wazembe na kuwa asingependa kuona ajali kama hizo.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE