March 24, 2018

AFISA MIPANGO MIJI MANISPAA YA IRINGA ACHONGEWA KWA RC IRINGA

Eneo la  uzio  iliyovunjwa  kinguvu 
Mafundi  wa  kiwanja  namba  tano  wakiwa kazini
eneo la  maegesho  ya gari  yaliyovunjwa kibabe
Hii  ndio  Transifoma  inayolalamikiwa  ambayo  imefungwa  eneo la kona barabarani na  eneo la maegesho ya gari ya  kiwanja  namba 6 
Mafundi  wakiendelea na  ujenzi

Eneo  lenye  mgogoro  hili hapa 
 ..........................................................................................................................................................................
Na  MatukiodaimaBlog 
MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  ameombwa  kuingilia  kati  sakata  la mgogoro  wa  kiwanja  namba 6  kitalu ‘P’ kilichopo  eneo la  stendi  kuu ya mabasi  baada ya  jirani wa  kiwanja  chicho  Aisen  Msigwa kuingia  kudaiwa  kujenga eneo la uchochoro.

Akizungmza na mwandishi  wa  habari  hizi  Jamila Abdallah  alisema  kuwa amekuwa  akifikisha  malalamiko  yake   juu ya ujenzi  unaoendelea  katika   eneo  hilo  pamoja na uwekaji  wa Transfoma ya  umeme eneo Uchochoro  eneo  ambalo ni hatari  kwa  usalama  ila hakuna  aliyemsikiliza  hivyo anaomba  mkuu  wa  mkoa wa Iringa kusaidia kumaliza mgogoro  huo .

Jamilla  alisema  kuwa  kitalu   hicho  kilichopo mtaa wa  Mahiwa kaya ya  Makorongoni  kimekuwa na mgogoro ambao  umesababishwa na jirani  yake  Msigwa  ambae ameendelea  anaendelea na  ujenzi  eneo hilo .

  Ni  muda  mrefu nilikwenda ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa  kumlalamikia afisa  mipango miji Bwana  Benda  ambae  amekuwa  akitumia  ubabe na  kutosikiliza malalamiko yangu  kwani  anatuonea na  kutunyanyasa sisi  wananchi  wanyonge  kwa  kumpendelea huyu  Msigwa ambae  anajenga  eneo  hilo  kibabe”

Alisema  jirani yake  huyo  mwenye kiwanja  namba  5 ameendelea  na  ujenzi katika  kichochoro  wakati  sheria za Manispaa  zinazuia wananchi  kuziba vichochoro .

Jamilla  alisema  kuwa kwa  unade wake  alijenga  uzio  kwa  kufuata taratibu  zote na  kibali  cha Manispaa ya  Iringa  toka mwaka 2006  na  kuwa anashangazwa  kuona jirani yake   huyo  anavunja  eneo  lake huku  akilindwa na  afisa   huyu .

Hata  hivyo  anasema kutokana na  jirani yake  kumtumia  ofisa  mipango  miji  anashangazwa  kuona  anapewa notisi na  kupigwa  faini  shilingi 200,000 kwa madai ya  kuziba  mfereji wa maji machafu  jambo  ambalo  si kweli kwani  ujenzi   wa uzio na  jengo lake  ulijengwa kwa  kufuata taratibu  zote  na wakaguzi wa Manispaa kabla  na  baada ya  ujenzi  walikagua  iweje  leo  kuibuka na hoja  kuwa mfereji  umezibwa  baada ya  kumlalamikia jirani yake  huyo.

Alisema  wakati  akijenga uzio  aliacha  mita 1.5 kwa  ajili ya  uchochoro  tangu  alipojenga  jengo hilo mwaka 2006 na mifereji  yote  ilikuwa  ikipitisha  maji na  wapiti  njia  walikuwa  wakipita vizuri  eneo hilo .

“ Kweli  inaumiza  sana kuona haya  yanaanza  kuibuka  sasa wakati  miaka  yote  sikupata  kupewa  notisi  yeyote   ile  ni  vema  Manispaa  ingefanya  uchunguzi  wa kina ungebaini  yote haya  kuanzia  mwaka 2016  mara  baada ya jirani huyo  mwenye  kiwanja namba 5 kuanza  ujenzi  wa jengo lake  ndipo  matatizo yameanza  na  kutufanya  kuishi  bila amani tunaona  tunavamiwa bila  taarifa  yeyote   msingi wa  nyumba  yangu  unachimbwa  kokoto  na mchanga umechukuliwa “

 Alisema  jirani yake  huyo  kwa  ubabe amevamia  na  kuziba  frontag ya jengo lake pamoja na eneo lake la maegesho ya  gari  kwa  kuweka  Transfoma yake  binafsi  kwa  ajili ya hoteli yake  huku akitambua  kuwa  kufanya  hivyo ni  kosa  jambo  ambalo  limepelekea  wapangaji wake  kuhama na kwenda  kupanga sehemu  nyingine .

Hivyo  anaomba  serikali  kumchunguza afisa  huyo  mipango  miji  kutokana na  kufanya kazi hiyo  kwa   upendeleo na  kukandamiza wanyonge  .

                    Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza akizungumzia  madai hayo amesema ameyapata  na  amemwagiza  mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa kusimamisha mara  moja  ujenzi  huo .

Pamoja na  mkuu  wa  mkoa  kuagiza ujenzi  huo  kusimama  bado  mwandishi  wa habari  hizi  alishuhudia ujenzi  huo  ukiendelea  jambo  ambalo  linaonyesha  ni upuuzaji  wa agizo la  mkuu wa  mkoa .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE