March 26, 2018

ABDULI NONDO AACHIWA KWA DHAMANA LEO

Nondo  akiwa na  wakili  wake kutoka  Dar (kulia)  wakitokea  magereza ya  Iringa baada ya  polisi  kumpeleka gerezani kabla ya  muda uliopangwa na mahakama wa  kukamilisha  dhamana  kumalizika
Abdul Nondo  akitolewa Mahabusu ya mahakama
Abdul Nondo akishangaa viwanja  vya mahakama  baada ya  kuachiwa  kwa  dhamana
Nondo  akiongea na  baadhi ya  wanafunzi  wenzake  toka  vyuo  vya Iringa
Nondo  akipanda  gari maalum  kurejea  Dar es Salaam  baada ya  kudhaminiwa leo 

Na  MatukiodaimaBlog 
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa Leo tarehe 26 March 2018 amemuachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania ndugu Abdul Nondo.

 Hakimu amefikia maamuzi hayo baada ya kueleza sababu mbali mbali ikiwemo haki aliyo nayo mtuhumiwa kuhesabiwa hana hatia hadi pale mahakama itakapoona ana hatia hivyo lazma apewe dhamana. 

Pia hakimu amesema kosa analotuhumiwa mtuhumiwa linadhaminika kwa mujibu wa sheria na hivyo hakuwa na sababu ya kuzuia dhamana...Mawakili wa upande wa Abdul Nondo, wakili Jebra Kambole na Chance Luoga walielekezwa na mahakama kutafuta wadhamini wawili; 


Mmoja wa serikali ambaye atasaini dhamana ya shilingi milioni tano na mwingine wa binafsi ambaye atasaini dhamana milioni tano pia wa binafsi alitakiwa kuwa na mali isiyohamishika yenye thamani ya milioni 5.

 Taratibu za wadhamini zilitakiwa kukamilika ndani ya muda wa masaa matatu. 

Hata hivyo kabla muda huo haujaisha Nondo alirudishwa Magereza na baadae kuletwa tena mahakamani ambapo wakili wa serikali aliomba muda wa lisaa limoja kujiridhisha na wadhamini. 

Baadae ndipo hakimu aliruhusu Nondo aachiwe huru kesi hiyo itakuja kwa ajili ya maelezo ya awali (Preliminary Hearing) tarehe 14.4. 2018 Nondo sasa yupo huru na taratibu za kumsafirisha kurudi Dar es Salaam kuendelea na masomo na shughuli zake zingine zinaendelea. 

Wakati huo huo leo mawakili wa upande wa Nondo wanategemea kupata majibu ya upande wa serikali katika maombi ya habeas corpus yaliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya 

Dar es Salaam ambapo pia mpeleka maombi aliiomba mahakama kutoa uamuzi juu ya uhalali wa polisi kumshikilia Nondo kwa takribani siku 16 kabla ya kupelekwa mahakamani Iringa


Kwa  upande  wake  Nondo  akizungumza nje ya  mahakama  baada ya  kuachiwa huru  alisema  kuwa anawashukuru  watanzania  wote  ambao  walikuwa  wakimuombea  pamoja na  vyombo vya  habari  vyote  kwa  ushirikiano mkubwa  alioonyeshwa .

Pia  Ndondo  alisema  kuwa hakuna  sehemu  yeyote  ambaye  alipata  kuandika  ama  kutoa maelezo kuwa  alitekwa .

“ Polisi  nikiwa Dar es Salaam  walikuwa wananihamisha mahabusu  za  polisi zaidi ya  mara tatu  wananitoa  mahabusu  hii  na  kunipeleka  mahabusu  nyingine hata  kuninyima  dhamana ambayo  ilikuwa ni  haki yangu  ila kweli  mahakama  imetenda  haki  hata  siamini kuona  nimepewa  dhamana “

Nondo  asema  ameishi  vizuri na  wenzake  magereza  na askari  Magereza Iringa anawashukuru  sana  maaana hawajanifanyia  ubaya  wowote ndio  maana  baada ya  kuachiwa  kwa  dhamana na mahakama  nimekwenda gerezani  kuwaaga  nimeagana  nao  vizuri   sana Mungu awabariki .

"  Naendelea  kumtegemea  Mwenyezi  Mungu  katika hili  maana na nimekuwa nazungushwa  kituo kimoja cha  polisi  hadi  kingine ila mfariji  wangu  ni  Mungu ndie  anayejua  ukweli katika   hili leo  nimepata  dhamana  ni  Mungu kanisaidia  hii ni hatua "

Ndondo ambaye  muda  wote  alikuwa  akilia  kwa  furaha ya  kuachiwa  kwa  dhamana hakuna  ndugu  hata  mmoja aliyefika mahakamani  hapo  zaidi ya  wanaharakati wa  mtandao  wa  watetezi  wa haki za  binadamu (THRDC),wanafunzi  wa  vyuo  vikuu Iringa  na wengine ameondoka  jana jioni  kurejea jijini  Dar es Salaam kuendelea  na mitihani yake aliyodai  inaanza   wiki  hii .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE