February 17, 2018

Wanajeshi wa DR Congo wauliwa na wenzao wa Rwanda

Mashariki mwa taifa la DR Congo karibu na mpaka na Rwanda ni eneo ambalo limekuwa halina udhibiti.

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMashariki mwa taifa la DR Congo karibu na mpaka na Rwanda ni eneo ambalo limekuwa halina udhibiti.
Wanajeshi watano wa DR Congo wameuawa na wanajeshi wa Rwanda kulingana na jeshi la nchi hiyo
Jenerali Bruno Mandevu alisema kuwa vita vilizuku katika mbuga ya wanyama ya Virunga katika ardhi ya Congo , madai ambayo Rwanda imekana.
Amesema kuwa wanajeshi wa Congo walidhania kwamba walikuwa wakikabiliana na waasi waliopo katika eneo hilo.
Wengine wanahofia kwamba mapigano huenda yakaongeza hali ya wasiwasi iliopo kati ya mataifa hayo mawili ambayo yana historia mbaya.
Rwanda iliwavamia mara mbili majirani zake 1990.
Msemaji wa jeshi la Rwanda kanali Innocent Munyengango alithibitisha kutokea kwa mashambuliano hayo na kusema hakukuwa na majeraha upande wa Rwanda.
''Jeshi la Congoleese lilivamia kambi yetu na kutushambulia. Wanajeshi wetu walilazimika kujitetea'', alisema.
Mashariki mwa taifa la DR Congo karibu na mpaka na Rwanda ni eneo ambalo limekuwa halina udhibiti.
Image captionMbuga ya wanyama pori ya Virunga DR Congo
Mashirika ya misaada yanaonya kutokea kwa ghasia katika mkoa wa Ituri uliopo Kaskazini mashariki, ambapo UNICEF inasema zaidi ya watoto 46,000 wametoroka.
Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga ameona vijiji vilivyochomwa katika mkoa huo ambapo watu kutoka makundi ya Hema na Lendu wamekuwa wakipigania udhibiti.
Mapema wiki hii, Baraza la wakimbizi nchini Norway limeonya kwamba mzozo nchini DR Congo unakaribua kutibuka.
Katika kipindi cha miaka miwili iliopita, watu zaidi wamewachwa bila makao nchini DR Congo zaidi ya nchi nyengine yoyote. Jumla ya watu milioni 4.5 wanaihitaji msaada

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE