February 23, 2018

WALIMU JIMBO LA VIRGINIA MAREKANI WAGOMA KUINGIA MADARASANI WAKILALAMIKIA MISHAHARA DUNI

  • Walimu jimbo la Virginia Marekani wagoma kuingia madarasani wakilalamikia mishahara duni

Mgomo wa walimu wa shule za jimbo la Virginia, magharibi mwa Marekani, umepelekea kufungwa shule zote za serikali na hivyo kuwakosesha masomo zaidi ya wanafunzi laki mbili jimboni hapo.

Gazeti la Washington Post limeandika kwamba, walimu wa jimbo lote la Virginia walianzisha mgomo jana Alkhamisi wakilalamikia mishahara midogo na marupurupu yao na walikataa kwenda mashuleni kuendelea na kazi yao. Katika mgomo huo walimu hao walikusanyika mbele ya jengo la bunge mjini Charleston, katikati ya jimbo hilo.
Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo walimu hao
Elissa Kiddy, Msemaji wa Wizara ya Elimu katika jimbo la Virginia amesema kuwa, kuanzia jana shule zote za jimbo hilo zilipigwa kufuli kutokana na mgomo humo wa walimu.

Huku mgomo huo ukiendelea hadi Ijumaa ya leo, afisa mkuu wa elimu wa jimbo hilo la magharibi mwa Marekani amekosoa mgomo huo na kusema kuwa unafanyika kinyume cha sheria. Kwa mujibu wa Umoja wa Walimu wa jimbo la Virginia, mishahara ya walimu wapya ni dola elfu 32 na 435 kwa mwaka huku kwa wale walimu wa zamani ikiwa ni dola elfu 44 na 701 kwa mwaka. 

Kwa mujibu wa walimu hao kiwango hicho cha mshahara ni kidogo mno ikilinganishwa na uhalisia wa maisha ya hivi sasa jimboni hapo, suala ambalo limewalazimimisha walimu wengi kuwa na maisha magumu kila siku.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE