February 22, 2018

WAKAZI WA MAGURUWE WAISHUKURU SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

Wakazi wa kijiji cha Maguruwe wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wameishukuru  serikali ya awamu ya tano kwa kuwathamini na kuweza kufika kwenye kijiji hicho mteule wa Rais ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, kwa kuwa hakuna kiongozi wa ngazi ya Uwaziri ambaye amewahi kufika kwenye eneo hilo.

Kutokana na Waziri Jafo kuwa Waziri wa kwanza kufika kwenye kijiji hicho wazee wa kimila wa kijiji hicho walimsimika na kumpa heshima maalum ya waluguru. 

Wakizungumza huku wakiwa wamejawa na furaha, Wananchi hao wamesema kijiji chao ambacho kipo juu kabisa ya safu za milima ya Ulugulu hakuna kiongozi yeyote wa ngazi  ya uwaziri aliyewahi kufika maeneo hayo kwa kuwa barabara zake hazipitiki kirahisi. 

Wamesema wamefurahishwa na kiongozi huyo kwa kuweza kuwafikia walipo hali ambayo imewafanya kujisikia furaha.

Katika ziara hiyo ya kikazi, Waziri Jafo amefanikiwa kuzindua vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa na Taasisi ya CDTF.

Hata hivyo, kutokana na changamoto kubwa ya barabara katika eneo hilo, Waziri Jafo alimuagiza meneja wa TARURA wilaya ya Mvomero kufanya tathmini ya barabara hiyo ili serikali ione jinsi ya kuifanyia kazi hapo baadae ili wananchi hao waweze kuondokana na adha hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE