February 15, 2018

UNYANYASAJI WA KINGONO WAITESA DUNIA

Kashfa kuhusu unyanyasaji wa kingono katika sekta ya misaada ya kigeni imeendelea kusambaa, baada ya shirika la Kifaransa la Madkari Wasio na Mipaka kujitokeza na ufichuzi mwingine
Shirika la Madktari Wasio na Mipaka maarufu kama MSF, limesema lilipokea malalamiko 146 mwaka jana, ambapo 40 kati ya malalamiko hayo yalipatikana kuwa tuhuma za unyanyasaji au mashambulizi ya kingono.
Imesema katika taarifa kuwa iliyachukulia hatua matukio 24 na kuwatimua wafanyakazi 19 baada a kufanya uchunguzi.
Huku ikiwa na karibu wahudumu 40,000 kote duniani, MSF ni moja ya mashirika makubwa ya misaada duniani, ikifahamika kwa kazi yake ya kutoa msaada wa matibabu katika maeneo ya migogoro.
Shirika hilo limesema kuwa hata ingawa ripoti za unyanyasaji zimeendelea kuongezeka, MSF inafahamu kuwa matukio hayo hayaripotiwi sana.
Oxfam Chief Executive Mark Goldring (L) und Oxfams Kuratoriumsvorsitzende Caroline Thomson (Getty Images/AFP/D. Leal-Olivas) Oxfam ilitangaza hatua dhidi ya unyanyasji wa kingono
Ufichuzi huo umefanywa wakati shirika la misaada la Uingereza Oxfam likikabiliwa na madai kuwa halikuwa wazi kuhusu kashfa inayowahusisha baadhi ya wahudumu wake kwa kuwatumia makahaba nchini Haiti kufuatia tetemeko kubwa la ardhi la mwaka wa 2010.
Kashfa hiyo ilisababisha kujiuzulu kwa naibu mkuu wa Oxfam na ikaibua suali kuhusu ufadhili wa shirika hilo kutoka kwa serikali ya Uingereza, ambao ulifikia pauni milioni 32 mwaka jana.  Uingereza imeonya jana kuwa huenda ikakata mahusiano na mashirika ya misaada ya kigeni ambayo yanaficha kashfa za unyanyasaji wa kingono.
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Penny Mordaunt aliyaelezea madai hayi ya ukahaba wa Haiti kuwa ya kutisha. aliwaambia wanahabari mjini Stockholm
Madai hayo yanamhusu aliyekuwa kiongozi wa ujumbe wa Oxfam nchini Haiti, raia wa Ubelgiji Roland van Hauwermeiren, ambaye tabia zake tayari zilikuwa zimesbabaisha mamaliko wakati akilifanyia kazi shirika hilo nchini Chad.
Baada ya kujiuzulu kutoka Oxfam, alienda kufanya kazi na shirika la Ufaransa la Action Against Hunger nchini Bangladesh. Oxfam imethibitisha ripoti kuwa mkurugenzi mwingine wa shirika hilo nchini Haiti, Damien Berrendorf, alifutwa kazi mwaka wa 2017 baada ya kuhudumu katika wadhifa huu kwa miaka kadhaa.
Uchunguzi wa ndani wa Oxfam kuhusu kuwatumia makahaba nchini Haiti ulisababisha kutimuliwa kwa wafanyakazi wane na wengine watatu wakaruhusiwa kujiuzulu akiwemo Van Hauwermeiren. Akizungumza na wanahabari mjini Stockholm waziri Mordaunt alisema washirika hilo liliwaacha watuhumiwa kuondoka bila kushitakiwa. Hawakuwafahamisha wafadhili, mamlaka za udhibiti au za mashtaka.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE