February 22, 2018

TECNO CAMON CM NA UBORA ILIYONAYO

Ni ukweli usiopingika kuwa TECNO, ni kampuni inayoendelea kufanya vyema katika uzalishaji na uuzaji wa simu janja barani Afrika hivi karibuni wamepokea mtazamo chanya kupitia toleo lao jipya Camon CM lenye sifa ya kuwa na kioo chenye wigo mpana.
1
Ufuatao ni uchambuzi baada ya kuifungua Camon CM
Camon CM imehifadhiwa vema kwenye kasha lenye sildi, ndani ya boksi nilikutana na chaji, vinasa sauti [earphone], lakini pia simu ina ulinzi wa kioo [screen protector],sambamba na kitabu kinachotoa maelezo kuhusu mipangilio ya simu na matumizi yake
2
Uwiano wa 18:9 ndo kitu kilichonivutia zaidi ambavyo nilikuwa natamani nipate simu yenye wigo mpana eneo la kioo, TECNO wameliwezesha hilo, ambapo Camon CM ina skrini yenye ukubwa wa inchi 5.7  ambapo niliweza kutazama filamu na kusoma habari mitandaoni kwa kuji nafasi pasipo kuwa  na mipaka ya kuta za simu.
3
Nilijipiga picha [selfie] zikatoka na ubora wa HD, kupitia 13 MP mbele na nyuma ikiambatana na flashi zake 4 ambazo hutoa mwanga kwa kuwaka waka  simu inapoita hivyo ni rahisi kugundua simu ikiita hata ikiwa umetoa muito
4
Nimehifadhi programu zaidi ya 80 nikiwa na 2GB RAM & 16 GB ROM  na bado nna nafasi ya kuweka memori kadi ya ziada kufikia GB 128, hivyo sina tena wasi wasi wa simu yangu kuzidiwa uwezo kwa kutokuwa na nafasi ya kuhhifadhi kumbkumbu na programu mbalimbali
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.tecnomobile.com/tz

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE