February 26, 2018

SUGU NA MASONGA WAHUKUMIWA JELA MIEZI MITANO

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamekutwa na hatia katika ya kesi inayowakabili na kutakiwa kwenda jela miezi mitano.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya HakimuMkazi Mbeya, Michael Mteite amesema kwamba washtakiwa hao wanapaswa kwenda jela kutokana na makosa waliyoyatenda katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya.
Kwa upande wa Washtakiwa Wakili Peter Kibatala aliyekuwa anamuwakilisha Sugu pamoja mwenzake aliiyomba mahakama hiyo iwapunguzie adhabu wateja waken kutokana na majukumu yanayowakabili ikiwepo la Sugu la kuwawakilisha wananchi bungeni.
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE