February 6, 2018

SERIKALI YATOA SIKU SABA KWA WANANCHI WALIOVAMIA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI YA JUKUMU KUONDOKA


  1. Baadhi wananchi wakiwasilikiliza Manaibu Waziri katika mkutano uliofanyiak jana katika  eneo la Mkesa  lililopo ndani ya Jumuiya ya  Hifadhi ya Wanyamapori  ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati wakati wa  ziara kutembelea  eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na  kujionea uharibifu unaoendelea katika .  

( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT) 


 
 
 

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na wa TAMISEMI  imetoa siku saba kwa wananchi  waliovamia kwa kuendesha maisha yao  na kufanya shughuli za kilimo pamoja   na kulisha mifugo  ndani ya  Jumuiya ya  Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU  iliyopo katika Halmashuri ya Morogoro vijijini  kuondoka katika hifadhi hiyo.
Hali hiyo inafuatia baada ya wananchi hao kwenda  mjini Dodoma kuonana na   Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa  na kumuelezea malalamiko yao kuwa wao ni wakazi  halali katika eneo hilo lakini hata hivyo    Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Regina Chonjo  amekuwa akiwalazimisha kuondoka. Kufuatia  hali  hiyo , Waziri Mkuu K Majaliwa  alimuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa TAMISEMI kwenda huko  kwa ajili ya kushughulikia tatizo hilo ambapo Mawaziri hao kutokana na kubwana  na majukumu mengine  waliwaagiza Manaibu  Waziri wao kutembelea eneo.  .
 

 


 

 

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda jana walitembelea eneo hilo na kujionea uharibifu unaoendelea.

 

 

Katika ziarz hiyo Manaibu Waziri hao walizungumza na  wananchi hao kwa  kumtaka mwananchi yeyote mwenye nyaraka halali za kuishi  katika eneo hilo aziwasilishe katika mkutano huo   lakini  hata hivyo hakuna mwananchi yeyote aliyeziwasilisha

.

 

Kutokana na wananchi hao  kukiri kuishi kinyume na sheria katika eneo hilo la Hifadhi,  Wananchi hao waliowaomba viongozi hao wapewe muda ili waweze kutafuta sehemu ya   kuhamia kwa vile hawana sehemu ya kwenda,

Kulingana uharibifu mkubwa waliojionea katika eneo hilo hali ya mazingira, Mnaaibu Waziri hao waliweza kuagiza mambo yafuatayo huyo. Kama.

 
Manaibu Waziri hao waliagiza kuwa materekta  yote yatakayoonekana katika eneo hilo la hifadhi baada ya siku saba kupita  yataifishwe.

 

 

Pia, Waliagiza kuwa  yakamatwe  na hatimaye kupigwa  mnada kwa mujibu wa sheria kwa mifugo yote itakayooneka  katika eneo hilo la  hifadhi

 

 

Aidha, Waliagiza kuwa  mwananchi yeyote atakayekutwa ndani ya hifadhi hiyo  baada ya siku saba kuwa atakamatwa na kufunguliwa  mashtaka kwa kosa la kuvamia hifadhi.

 

 

Awali, Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo   aliwaeleza Manaibu Waziri hao kuwa wananchi hao  wamekuwa wakilima na kuchunga mifugo katika  maeneo hayo  hali iliyopelekea wanyamapori katika maeneo hayo kuhama.

 

 

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya JUKUMU, Shaban Kolahili  ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii iwasaidie kuhakikisha kuwa hifadhi hhiyo inalindwa ili kuzuia vitendo vya ujangili na uvamizi unaoendelea ili kuwavutia wawekezaji ili hatimaye iweze kujitegemea.

 

 

Wananchi wa  eneo hilo  mnamo  mwaka 2010  walituma maombi  kwa Wizara ya Maliasili na Utalii  ya  kuomba  wasaidiwe katika kulihifadhi  eneo hilo  ambalo hutumiwa na wanyapori kupimzika na kuzaliana

 

 

 

 

 

 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE