February 5, 2018

SERIKALI YAHOJIWA KUHUSU MADAKTARI NA DAWA


maxresdefault
MBUNGE wa Geita Mjini,Costantine Kanyasu (CCM) amehoji  hatua ambazo serikali inachukua kuhakikisha kuwa dawa na madakaktari wa kutosha wanapakuwepo katika hopspitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita kwani ina uhaba wa dawa na madaktari.
Akijibu swali swali hilo,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,alisema hospitali ya Geita kwa Mwaka 2015 ilitengewa kiasi cha shilingi 141,937,184 na kwa Mwaka 2016-17 ilipokea shilingi 278,666,525 kiasi ambacho ni mara mbili ya mgao wa Mwaka wa fedha 2015-16.

“Katika Mwaka wa fedha 2017/18 hospitali hii baada ya kupandishwa hadhi kuwa ya Rufaa mgao wake umeongezeka na kufikia kiasi cha shilingi 368,287,841 na hadi kufikia mwezi Desemba mwaka 2017 hospitali hii imekuwa ikipokea kiasi cha shilingi 168,609,586.94 kwa ajili ya kununulia dawa kupitia bohari ya dawa,hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa katika hospitali hiyo ni asilimia 90 kwa dawa muhimu’’alisema Dr Ndungulile

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE