February 10, 2018

SERIKALI YA DKT MAGUFULI NI YA WATU KUFANYA KAZI SIO YA KUPIGA DILI - MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​
MAKAMU   wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan asema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imeziba mianya ya Rushwa na wizi kwa wapiga dili.

Hivyo awataka watanzania kufanya kazi halali zitakazo wawezesha kupata kipato sahihi kwani pesa za dili hazipo tena.

alisema kuwa wilaya hiyo Akizungumza jana na watumishi wa wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa halmashauri baada ya kutembelea wilaya hiyo alisema   wilaya ya Kilolo ni moja kati ya wilaya tajiri nchini ila kama kila mmoja atafanya kazi.

"Nipongeze maendeleo makubwa yaliyopo sasa zamani mlilala mkisubiri kila jambo kufanywa na serikali ila sasa mnafanya kazi kwa kipindi kifupi mmefanya Mengi"

Makamu huyo wa Rais alitaka kila mmoja kufanya kazi na kuacha wizi kwani serikali ya Dkt Magufuli imeziba mianya ya rushwa na ukwepaji kodi.

Alisema kuwa ununuzi wa gari la wagonjwa na ujenzi wa Hospitali ni kazi ya wilaya na mbunge na wadau wengine ila serikali inawezesha pale palipo kwama.

"Kuhusu kero ya barabara hii naichukua na ujenzi wake utakamilika ndani ya kipindi chetu kuoana inajengwa kwani ipo katika ilani ya uchaguzi na masuala ya afya ,elimu na maji tutayabeba kwa nguvu zote"


Alisema afya,maji ,elimu na umeme vijijini na miundo mbinu inayojenga uchumi wa kitaifa yote yatakwenda kwa nguvu kubwa zaidi.

"Kitakachowezesha uchumi wa viwanda unakuzwa zaidi ni kuona sekta hiyo inaboreshwa ili kuongeza uzalishaji kwa wakulima"

Hata hivyo alionya madiwani na viongozi wa kuchaguliwa kuacha kufanya kazi ili kupata pesa isipo kuwa kufanya kazi kwa kuwatumikia wananchi.

Kuhusu mkakati wa wilaya ya Kilolo kuanzisha kilimo cha Parachichi alisema jambo hilo linaungwa mkono na serikali kwani litakuza uchumi wa wananchi pamoja na zao la korosho.

Akisoma taarifa ya wilaya ya wilaya ya Kilolo mkuu wa wilaya hiyo Asia Abdalah alisema wilaya hiyo  inaomba kiasi cha zaidi ya  shilingi bilioni 4.5  kwa ajili ya ukamilishaji wa Hospitali ya wilaya hiyo.

Alisema  wilaya    hiyo  ina jumla ya  vituo  61 vya  kutolea  huduma  za afya  ikiwa  ni pamoja na  Zahanati 58 na vituo  vya afya  viwili na  Hospitali  teule  ya  Ilula .

" Kuanza  kwa  ujenzi  wa miundo mbinu  muhimu ya  Hospitali ya wilaya  hadi  sasa  jengo la  wagonjwa  wa  nje ,jengo la  kulaza   wagonjwa ,jengo la  mionzi ,jengo la maabara  na  jengo la  mama  na  mtoto  limejengwa  na serikali  imetoa bilioni 1.5  kati ya  bilioni 4.5 zinazohitajika kukamilisha  ujenzi  huo"

Aidha   wilaya  imepokea  kiasi cha  shilingi milioni 400 kwa  ajili ya  ukarabati  wa  kituo cha afya KIdabaga  na  jamii  husika  imeshirikishwa  kutekeleza mradi huo .

Kuwa kutolewa kwa kiasi hicho cha pesa kutasaidia wilaya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ambao unaendelea.

Hata hivyo aliomba serikali kuweza kusaidia kutatua kero ya miundo mbinu ya barabara katika wilaya hiyo ambayo inakwamisha ukuaji wa uchumi wa wilaya ya Kilolo.

Katika kuhakikisha wananchi wanazidi kukuwa kiuchumi serikali ya wilaya imejipanga kufufua kiwanda cha chai Kidabaga pamoja na kuendeleza uanzishwaji wa viwanda zaidi katika wilaya hiyo.


Kuhusu kero ya maji alisema jitihada za kukamilisha mradi mkubwa wa maji Mji wa Ilula zinafanyika na ukiamilika mradi huo kero ya maji ilula itakuwa ni histori.

Asia alisema wilaya imeweka mkazo wa kuanzisha kilimo cha Parachichi na kilimo cha zao la korosho na kufufua zao la Pareto .

"Tunaimani kubwa na utendaji kazi wa serikali ya Rais Dkt John Magufuli na wewe mwenyewe makamu wa Rais kazi mnayoifanya ni kubwa zaidi na imani yetu kuona changamoto ya barabara inatatuliwa"

Mkuu huyo wa wilaya alisema mbali ya serikali kufanya jitihada kubwa za kuleta maendeleo wilaya ya Kilolo ila kuna wadau mbali mbali ambao wamekuwa ni chachu ya maendeleo ya Kilolo akiwemo mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Salim Asas kupitia kampuni yake ya Asas Group ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Kilolo.

Hivyo alisema kuwa iwapo wilaya hiyo itasaidiwa kutengenezewa barabara ya Lami urefu wa kilomita kama 25 hadi Ipogolo mjini Iringa kero za wananchi juu ya barabara zitakwisha.


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa changamoto kubwa ni barabara na kama serikali itasaidia kutatua kero hiyo basi wilaya hiyo itakuwa imefunguka kiuchumi.

Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto alisema kuwa pamoja na changamoto nyingine wananchi wanalalamika suala la gharama kubwa ya pembejeo za Kilolo hasa mbolea ambayo bei yake ni kubwa zaidi  ukilinganisha  na  bei  ilekezi ya  serikali .

Pia suala la wananchi kupata huduma ya kuni kwa kibali na changamoto ya miundo mbinu.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE