February 10, 2018

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAPONGEZA WILAYA YA KILOLO KUPATA HATI SAFI ,YAPONGEZA KAMPUNI YA ASAS GROUP KWA MICHANGO MBALI MBALI

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akisoma taarifa ya wilaya yake mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati ziara ya Makamu wa Rais wilayani Kilolo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Wilaya ya Kilolo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (kulia) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas.

 Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari ya Kilolo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Na  MatukiodaimaBlog

SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imepongeza halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kwa kupata hati safi kuiendesha vema wilaya   hiyo   kimaendeleo .

Pamoja na ponngezi hizo kutoka Kwa Rais Dkt Magufuli pia amepongeza msaada mkubwa wa maendeleo unaofanywa na kampuni ya Asas Group .

Akizungumza Leo katika mji wa Ilula wakati akiwahutubia wananchi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alisema Rais Dkt Magufuli amevutiwa na utendaji kazi mzuri wa Halmashauri ya Kilolo pia jitihada za Asas Group .

Alisema katika kuongeza mapato halmashauri hiyo imeweza kukusanya vizuri mapato yake na kuagiza kuongeza zaidi ukusanyaji wa mapato.

"Nimetoka wilayani tumeambia wananchi wananyasika kwa kodi za mbao na kuni za kutumia nyumbani kweli kuna tatizo kuni za matumizi ya nyumbani si sahihi kutoza kodi ila kama ni kuni au mbao za biashara lazima mlipe kodi"

Hivyo alitaka jamii ili kusukuma maendeleo no lazima kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.


Kuhusu kero ya maji Ilula alisema serikali inaendelea kuboresha Huduma ya maji katika mji wa Ilula na itaendelea kuboresha zaidi huduma ya maji .

Makamu wa Rais ameipongeza wilaya ya Kilolo kwa kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi na kuagiza zoezi la upimaji wa vijiji kuendelea zaidi ili kuondoa migogoro ya ardhi kati ya kijiji na kijiji.

Aidha alisema pamoja na changamoto mbali mbali zilizopo baadhi ya changamoto zinakwamishwa na baadhi ya watumishi kuleta vikwazo kwa mvutano wa kisiasa.


Kuwa wakati meingine serikali inaleta pesa kwa ajili ya maendeleo ila wapo baadhi ya watu wachache wanaokwamisha matumizi ya pesa hizo naombeni kuletewa watu hao.

Kuhusu changamoto ya gari la wagonjwa alisema anaipongeza halmashauri kwa kutenga bajeti ya ununua gari na kwa upande wake na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto wataangalia uwezekano wa kuongeza gari.

"Pamoja na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Rais Dkt Magufuli wapo ambao wanapita chini chini kuhujumu jitihada hizo jambo ambalo serikali haitafumbia macho wanaokwamisha jitihada za serikali wachukulieni hatua watu hao msisubiri Waziri mkuu aje"

Pia makamu wa Rais amepongeza jitihada za serikali ya Mkoa wa Iringa kwa kuonyesha mkakati mzuri wa kuanzisha viwanda na kuwa serikali imeendelea kutekeleza usogezaji wa umeme na Mara mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu utakapo malizika vijiji vyote Mkoa wa Iringa vitapata umeme.

Kuwa wakati serikali inaendelea kuwatumikia wananchi no vema wananchi kuendelea kuombea amani nchini pamoja na kulinda amani na asiwepo mtu wa kuvuruga amani ya taifa.

Kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Salim Abri Asas akiahidi   kwa  niaba ya  CCM  mkoa  kuchangia  bati  500 na  saruji  mifuko  300  ili kumuunga mkono makamu wa Rais  aliyechangia milioni 5 kuendeleza elimu kilolo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE