February 12, 2018

SALAMU ZA MKUU WA MKOA WA IRINGA WAKATI WA UZINDUZI WA MRADI WA REGROW – IRINGATAREHE 12/02/2018

Image result for rc iringa Samia Suluhu  Hassan

Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu aliyekuwezesha wewe pamoja na wageni wote kusafiri salama hadi Mkoani Iringa.
Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Iringa, tunayo furaha kubwa kukukaribisha wewe pamoja na wageni wote.
Tunafarijika sana kwa ujio wenu na tunasema karibu sana Mkoani Iringa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Wananchi wa Mkoa wa Iringa, wanayofuraha kubwa sana, na wanatoa shukrani zao za dhati kwa Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwaletea miradi mbalimbali ambayo inayotekelezwa  Mkoani Iringa. Kipekee wanashukuru sana ujio wa mradi wa REGROW ambao utachochea ukuaji wa Utalii ukanda wa Kusini kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Mkoa wa Iringa uliteuliwa kuwa kitovu cha Utalii kwa Mikoa ya Kusini na Wizara ya Maliasili na Utalii Mwaka 2009 ambapo maonyesho ya kwanza ya Utalii - kitaifa yalifanyika Mkoani Iringa. Kwa msingi huo Mwaka 2015, 2016, 1017 Mkoa umekuwa ukifanya maonyesho ya Utalii ambayo yanajumuisha  Mikoa mingine ya kusini na yanaitwaKARIBU KUSINI.


Mhe makamu wa Rais
Maandalizi ya Maonesho ya karibu kusini mwaka huu 2018 yameanza na Mkoa umedhamiria maonesho haya yafanyike kwenye eneo hili ambalo litakuwa maalum kwa ajili ya maonesho ya Utalii ya KARIBU KUSINI.
Katika kuhakikisha tunafanikiwa; tayari tumeunda kamati ya Utalii ngazi ya Mkoa na Wilaya na  tumeamua kuwa suala la Utalii ni agenda ya kudumu. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Mradi huu, ni fursa kwetu na tunaamini tutaendelea kwa kasi zaidi kwenye Sekta ya Utalii na uhifadhi kwa ujumla; na hivyo kutimiza azma ya Serikali ya kufungua utalii Mikoa ya kusini.

Mheshimiwa Makamu wa Rais,
Baada ya maelezo haya mafupi sasa naomba kuwatambulisha Wageni mbalimbali waliopo hapa.


B: Viongozi ngazi ya Mkoa:
1.      Wakuu wa Mikoa
2.      Makatibu tawala wa Mikoa,
3.      Mwenyekiti wa CCM
4.      Mjumbe wa Siasa Mkoa
5.      Wahe. Wabunge
6.      KUU (Mkoa na Wilaya)
7.      Viongozi wa Dini
8.      Wahe. Majaji
9.      Wakuu wa Wilaya
10.                Wakuu wa Vyuo (RUCU, MKWAWA, IRINGA, OPEN)
11.                Wapo Viongozi wa Taasisi Mbalimbali (taasisi za Umma, na taasisi binafsi)
12.                Viongozi wa Vyama vya Siasa,


13.                Baada ya Utambulisho huu, Namwomba Waziri wa maliasili naye aje atoe utambulisho kwa Ngazi ya Kitaifa

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE