February 2, 2018

RAIS MAGUFULI AKABIDHI BAJAJI ALIYOAHIDI


bj2
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Gerson Msigwa wakimwongoza mlemavu wa maungo Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga kwenye Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018
bj3
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi  mlemavu wa maungo  Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. Kulia ni ke w Bw. Ndemanga, Bi. Hawa Mohamed.
bj4
bj5
mlemavu wa maungo  Bw. Yusuf Abdulrahman Ndemanga na mkewe Hawa Mohamed Wakiondoka na Bajaji ambayo aliahidiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli walipokutana wakati wanavuka kwenye pantoni ya MV Kigamboni Agosti 25, mwaka jana, kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 2, 2018. 
6-3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Abdulrahman Ndemanga ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam Agosti 25, mwaka jana. Bw. Ndemanga alimuomba Rais msada wa kupatiwa Bajaji ili ajimudu kiusafiri na kiuchumi.
Picha na IKULU

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE